KIUNGO Mshambuliaji wa Yanga, Denis Nkane amefunguka kuwa malengo yake makubwa ni kucheza ligi ya La Liga.

Nkane ambaye amekuwa na msimu bora alijiunga na Yanga kwenye dirisha dogo la usajili msimu huu akitokea Biashara United ya Mara.

 

nkane, Nkane: Natamani kucheza La Liga., Meridianbet

Akizungumzia malengo yake kinda huyo amesema kuwa “Nilipoingia Yanga nilikuja kwa kuwa na malengo makubwa ambayo ni ya kuhakikisha nafikia mipango yangu.

“Nilifikiria kwamba nikiwa Yanga kwa sababu ni timu kubwa inayojulikana Afrika na duniani basi itakuwa ni sehemu sahihi kwa upande wangu.
“Tangu nikiwa mdogo nilijiwekea malengo yangu ambayo ni kuhakikisha nacheza La Liga hivyo natumia nafasi hii vizuri ili niweze kutimiza yale nilijiwekea.”

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa