Soka la sasa linatawaliwa na vijana wenye uwezo wa kipekee kwenye nafasi zao. Christopher Nkunku ni miongoni mwao, kumsajili kunamahesabu yanahitajika.

Kwa sasa anakipiga nchini Ujerumani akiwa na RB Leipzig. Umri wake ni miaka 24 tu na kwa kwa msimu huu, ameshapachika magoli 31 kwenye michuano yote waliyocheza.

Bila shaka, PSG wanakuna vichwa wakiwaza na kuwazua maamuzi yao ya kumuuza Nkunku. Sasa hivi, anahusishwa na vilabu kadhaa barani Ulaya kuelekea ufunguzi wa dirisha kubwa la usajili.

Leipzig nao pia wanamipango yao. Hapa ni mchezo wa pata potea, mahesabu makali yanahitajika kwa pande zote zinazohusika katika mchakato wa usajili wake.

Nkunku, Nkunku: Mahesabu Yanahitajika., Meridianbet

Leipzig wanaamini wananafasi ya kumsainisha mkataba mpya na kuweka kipengele cha kumuuza kwa dau la £54.8M mwishoni mwa msimu ujao. Hii ikiwa na maana kuwa, wanataka kumbakiza klabuni hapo wakiwa na lengo la kupambana vikali na Bayern Munich msimu ujao na, watakua tayari kumuachia msimu ujao ukiisha.

Upande wa pili, kwa timu inayomtaka Nkunku mwishoni mwa msimu huu, basi itapaswa kutoa pesa ndefu (hana kipengele cha dau maalumu la kumuuza) zaidi inakadiriwa kuwa ni £80M. Ni tofauti ya takribani £25.2M kumsajili msimu huu au ujao.

Waswahili wanasema – “akili kumkichwa”.


TENGENEZA FAIDA NA ZEUS ANCIENT FORTUNES

Una Kila sababu ya kufurahia wiki yako na kutengeneza mwaka huu uwe wa faida zaidi katika kasino zetu za mtandaoni za meridianbettz. Mchezo wa Zeus Ancient Fortunes unakuongoza kutekeleza hilo.

tetesi, Tetesi za Soka Barani Ulaya., Meridianbet

CHEZA HAPA

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa