Norwich Inajiweka Sawa Kwa Msimu Ujao.

Baada ya kushuka daraja msimu wa 2019/20, Norwich City sasa wanarejea kwenye EPL msimu ujao, 2021/22.

Vijana wa Carrow Road wanaendelea kujiweka sawa kuelekea msimu ujao. Norwich wameshamrudisha kwenye timu hiyo aliyewahi kuwa kipa wa timu hiyo, Angus Gunn aliyekuwa anaitumikia Southampton msimu uliopita. Gunn amesaini mkataba wa miaka 4 kuwepo Carrow Road.

Sambamba na Gunn, klabu hii inahusishwa na mpango wa kumsajili kinda wa Chelsea, Billy Gilmour. Gilmour amekuwa kwenye kiwango thabiti akiwa na timu ya Taifa ya Scotland kunako mashindano ya Euro 2020.

Licha ya Scotland kutolewa kwenye mashindano ikiwa ni hatua ya makundi tu, Gilmour ameonesha uwezo wake wa kutawala uwanja kwenye safu ya kiungo. Imeripotiwa vigogo wa Cannaries wanampango wa kumsajili Gilmour kwa mkataba wa mkopo wa msimu mmoja.


USHINDI BILA MIPAKA!

Hakuna mipaka ya ushindi kwenye Keno Instant ya meridianbet Kasino, hii wewe ndiyo una uamuzi zaidi juu ya mchezo na nafasi ya machaguo kibao.
Arsenal, Arsenal Wawasilisha Ofa ya Pili Joaquin Correa., Meridianbet

Acha ujumbe