Klabu ya Nottingahm Forest imetuma maombi kwa klabu ya Manchester United ya kumuhitaji winga wa klabu hiyo Anthony Elanga kwa mkopo wa msimu mzima.
Nottingham Forest wanamuhitaji winga Elanga kwajili ya kuimarisha upana wa kikosi chao kuelekea msimu ujao wa ligi kuu ya Uingereza, Huku vilevile wakimuhitaji golikipa wa klabu hiyo Dean Henderson ambao alikua klabuni hapo msimu uliomalizika.Klabu ya Man United inaarifiwa kwenye mpango na winga Anthony Elanga hivo klabu hiyo inataka kutumia faida ya kumpata mchezaji huyo kutokana na kutokua kwenye mipango ya klabu ya Manchester United chini ya kocha Ten Hag.
Nottingham Forest wanataka kuwapata wachezaji hao wawili kutoka klabu ya Manchester United ambapo Dean Henderson aliitumikia klabu hiyo msimu uliomalizika kabla ya kupata majeraha na sasa wanataka kumnunua kwa uhamisho wa kudumu.Manchester United wanatarajia kupokea ofa nzuri kwa golikipa Dean Henderson ili waweze kumuachia kipa huyo kuelekea Nottingham Forest, Huku kwa Elanga mazungumzo ya mkopo bado yanaendelea.