Novak Djokovic anatarajia kuanza maandalizi ya kutetea taji lake la French Open mwezi ujao kwenye hafla ya ATP Masters kwenye uwanja wa Monte Carlo.
Mshindi huyo mara 20 wa Grand Slam hakuweza kutetea taji lake la wazi la Australian Open mwezi Januari baada ya kufukuzwa nchini kwa ghasia baada ya kuruhusiwa kushiriki michuano hiyo licha ya kutopewa chanjo ya virusi vya corona.
Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 34 pia atakosa mashindano ya mwezi huu ya ATP 1000 huko Indian Wells na Miami, na hawezi kuingia Marekani bila uthibitisho wa chanjo.
Huko Monaco anakoishi Djokovic wanaruhusu wasafiri wa kimataifa kuonyesha uthibitisho wa kupona Covid-19 miezi sita iliyopita. Djokovic amesema alipimwa na kukutwa na virusi hivyo kwa mara ya pili mwezi Desemba.
“Novak atafungua msimu wake wa 2022 huko Monte Carlo, ambako alishinda taji la Masters 1000 mara mbili, mnamo 2013 na 2015,” taarifa kutoka wavuti yake iliandika.
Monte Carlo Masters, ambayo itaanza Aprili 10 hadi 17, itakuwa michuano ya pili katika msimu wa 2022 kwa Djokovic, ambaye alipoteza katika robo fainali ya tukio la ATP 500 huko Dubai mwezi uliopita.
Kwa sasa Djokovic ameorodheshwa namba 2 kwa ubora duniani baada ya kupoteza nafasi yake ya kwanza kwa Daniil Medvedev wiki iliyopita.
Mchongo mpya mjini ni Shindano la Evoplay Spring Aweking katika kasino maridhawa za meridianbettz. Pata mgao wako wa TSh 25,000,000 katika michezo kibao ya kasino na sloti ziliyochaguliwa kushiriki.