Novatus Dismas, Kumbuka Walikuwepo na Sasa Hawapo

Novatus Kaka! Shika simu yangu, ingia kwenye Notebook yangu kuna majina nimeandika hapo, hayo yote ni kwa ajili yako maana tunaishi kwa mifano, hilo jina la kwanza ni Renato Sanchez wa Ureno

Huyo Mtoto alikuwa Golden boy 2016, dunia yote ilikuwa miguuni mwake bahati mbaya sana presha ikambeba, uzito wa jina ukamuhukumu mwisho ukubwa wa Bayern Munich ukapigilia msumari wa mwisho, najua unakumbuka kilichotokea

Nenda na jina la pili hapo, umesema ni Bojan Kirkic Perez! Naam pale Joan Gamper Barcelona alikuwa anafanya mazoezi pembeni ya Lionel Messi, alifanya maajabu makubwa na dunia ikamsubiri

Alifunga kila weekend pale Camp Nou, alicheza atakavyo na tukaamini La Masia imeleta kitu, ila ujana maji ya moto bwana Novatus, mtoto huyu ukubwa wa jina lake ukamchukua, akili ikajifumba maisha yaliisha alivyotoka tu Camp Nou

Umesema umeliona jina lingine hapo la Kylian Mbappe! Naam huyu dunia ilianza kuwa chini ya miguu yake tangu Monaco akaitwa The Second Prince, licha ya ukubwa wake alikuwa analala hostel na kudamka mazoezini

Leo hii Mbappe kashinda vingi lakini bado anahitaji vingi, ukubwa wa jina lake kauficha nyuma, bado anajiona Mbappe mtoto mdogo asie na kitu kwenye dunia, Bwana Novatus kuna somo hapa

Nisiwe muongeaji sana, kwa Renato nakupa somo utaanguka ila futa vumbi simama tena, kwa Bojan ni majuto ni mjukuu na kwa Mbappe ni endelea kupambana kuwa jua ili ukidondoka uwe nyota tu.


USHUJAA UNAKULIPA HAPA!

Hii ni halisi kwa ajili ya mashujaa wote! Ukiwa jasiri unavuna mkwanja kibao hapa na sloti hii ya Huangdi Casino. Waka nusu tukupe maradufu!

Ratiba ya Soka Ligi Mbalimbali.

Ingia Mchezoni!

16 Komentara

    The meridian bet kwa makala nzuri ya kispoti ya wasihiii wachezaj wetu kuwa na nidhamu katika maisha ya soka kwani muda haumsubir mtu na majuto baadaye sana

    Jibu

    Kabsaa yaan

    Jibu

    Ni kweli kabisa yani

    Jibu

    Mpira ni kujituma sana ili ufike unapotaka

    Jibu

    Mwandishi ameongea uharisia kabisa Sanchez ni kiboko mwaka huo

    Jibu

    Ndo mana kwenye suala la mpira unatakiwa kujituma sana ukiwa bado unanguvu

    Jibu

    Soka c kitu cha masihara ni kujitoa mazima

    Jibu

    Sahihi kabisa

    Jibu

    Mashabiki tumeielewa makala

    Jibu

    Mpira ni kujituma sana ukiwa uwanjani hili kureta hamsha hamsha kwa mashabiki

    Jibu

    Alichosema Novatus ni sahihi kabisa

    Jibu

    Nikweli mpira ni kujituma na nidhamu ni ndio kila kitu

    Jibu

    Mpira Ni kujituma na kuweka nidhamu ya kutosh nje ya uwanj na ndan pia

    Jibu

    Asante sana kwa uchambuzi yakinifu

    Jibu

    Mchezaj anatakiw ajitume zaid

    Jibu

    Good

    Jibu

Acha ujumbe