Nunez Aiua Leicester Ipswich Ikifuzu Raundi ya Tatu

Marcelino Nunez amekuwa shujaa wa Ipswich Town baada ya kufunga mabao mawili, likiwemo moja la kushangaza kutoka umbali wa takribani yadi 45, na kuisaidia timu hiyo ya kuichapa Leicester City na kutinga raundi ya tatu ya Carabao Cup. Nunez alifanya usiku wa Portman Road kuwa wa kipekee baada ya kuonyesha ubora wa hali ya juu, huku bao lake la pili likiwa gumzo kubwa zaidi. Ipswich ilifanikiwa kupata ushindi uliokuwa mgumu licha ya Leicester kutawala sehemu kubwa ya mchezo.

Nunez Aiua Leicester Ipswich Ikifuzu Raundi ya Tatu

Bao lake la kuhitimisha lilikuja katika dakika ya kwanza ya muda wa nyongeza kipindi cha pili. Nunez alikuwa katikati ya uwanja, alipomwona kipa Jakub Stolarczyk akiwa ametoka mbali na lango lake. Bila kusita, kiungo huyo alifyatua kombora kutoka umbali wa takribani yadi 45, mpira ukampita kipa na kugonga upande wa chini wa mwamba wa juu kabla ya kutinga wavuni. Lilikuwa bao la aina yake, lile ambalo mashabiki walikuwa bado wakilitafakari hata baada ya filimbi ya mwisho.

Bila kusahau meridianbet ndio wakali wa ODDS KUBWA, Machaguo zaidi ya 1000 na kila kitu ukitakacho. Bashiri kijanja hapa

Leicester ilianza kwa kasi na ilikuwa na nafasi kadhaa za kuandika historia yake. Tom Watson alikaribia kufunga baada ya Christian Walton kufanya kosa la kumpa mpira mpinzani kwa uzembe, lakini kipa huyo wa Ipswich alijirekebisha kwa kufanya sevu nzuri dhidi ya Christian McFarlane. Leicester pia ilidhani imepata bao baada ya Kasey McAteer kufuatilia mpira uliodondoshwa na Stolarczyk kufuatia kichwa cha Dara O’Shea, lakini bao hilo lilikataliwa kwa sababu ya kuotea. Conor Chaplin, ambaye aliwahi kuitumikia Ipswich kwa miaka mitano kabla ya kuondoka bure msimu huu, pia alipata nafasi ya kuwapa Leicester uongozi kupitia mpira wa adhabu, lakini shuti lake liligonga ukuta.

Nunez Aiua Leicester Ipswich Ikifuzu Raundi ya Tatu

Ipswich hatimaye ilivunja ukuta wa Leicester dakika ya 62. Chuba Akpom alifanya kazi nzuri ya kuushikilia mpira kabla ya kumwachia Jack Clarke, ambaye alipeleka krosi nzuri kutoka upande wa kushoto. Sindre Walle Egeli alikuwa huru ndani ya eneo la hatari na hakufanya makosa, akimalizia kwa utulivu na kuifanya Ipswich kuongoza. Lakini Leicester ilijibu haraka, kwani dakika tano baadaye Olabade Aluko mwenye miaka 19 alisukuma mpira wavuni kutoka karibu baada ya kichwa cha Bobby De Cordova Reid kuelekezwa langoni. Mchezo ukawa wazi tena, lakini Nunez alikuwa bado hajamaliza kazi yake.

Nunez Aiua Leicester Ipswich Ikifuzu Raundi ya Tatu

Dakika ya 71, Nunez alirejea tena kwenye ubao wa mabao baada ya kufunga kutoka nje ya eneo la hatari, huku Akpom akihusika tena katika maandalizi ya shambulizi hilo. Leicester ilijaribu kusaka bao la kusawazisha, huku Will Alves akipiga shuti lililokwenda nje, lakini kila kitu kikaangukia mikononi mwa Nunez. Kombora lake la yadi 45 likafunga mjadala, likaipeleka Ipswich kwenye raundi ya tatu ya Carabao Cup na kwenye droo ya Jumatano.

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.