Golikipa wa timu ya Atletico Madrid, Jan Oblak ameibuka kuwa mchezaji bora wa ligi kuu ya Hispania kwa msimu wa 2020/2021.
Siku kadhaa tu zilizopita Oblak alitangazwa kuwa kipa bora wa msimu, akiwa na clean sheets 18, huku amejitengezea 80% za kuokoa michomo langoni mwake.
Tuzo ya mchezaji bora wa Laliga ilikuwa ikionekana kupambaniwa na wachezaji mbalimbali kama vile Lionel Messi, Suarez, Moreno na Benzema. Lakini wote walikufa kibudu mbele ya golikipa huyo.
Katika msimu huu, Oblak aliokoa penati tatu kati ya nne alizokutananazo ili kujihakikishia anaokoa sana na kuisaidia timu yake inafanya makubwa na hatimaye akasaidia kubeba ndoo mbele ya Madrid.
Mchezaji mwingine alikuwa akitazamiwa sana kubeba tuzo hiyo ni Lionel Messi, ambaye ameibuka mfungaji bora licha ya kuwa na msimu mbovu pale Camp Neu akiweka kambani magoli 30.
Wengineo ni Benzema wa Madrid na Moreno wa Villareal ambao wote kwa pamoja walitupia kamba 23 na kuibuka vinara wa ufungaji klabuni mwao sambamba na Suarez licha ya kuachwa na Barcelona!
Chukua namba yako ya akaunti na kiasi cha pesa unachotaka kuweka, sogea kwenye duka lolote la Meridianbet lililo karibu nawe utasaidiwa kuweka pesa.
Hongera zake