Golikipa wa Atletico Madrid Jan Oblak anaamini kuwa mashabiki zao wa Atletico Madrid “wanastahili zaidi” baada ya timu yao kuondolewa kwenye Ligi ya Mabingwa hapo jana.

 

Oblak Awaomba Radhi Mashabiki Zao kwa Kushindwa Kufuzu 16 Bora

Oblak amesisitiza kuwa timu hiyo inatakiwa ichukue jukumu la kufanya vizuri kwenye mechi yao ya mwisho ambayo ni ya muhimu itakayowawezesha wacheze michuano ya Europa baada ya hapo jana kushindwa kupata ushindi mbele ya Leverkusen kwa kwemda sare ya 2-2, huku Carrasco akishindwa kuibeba timu hiyo kwa kukosa penati katika dakika ya 90+9 ya mchezo.

Oblak amesema kuwa; “Ni ukatili sana kuondolewa. Ni soka, tumefanya kila kitu kushinda, lakini michezo iliyopita imetuadhibu, hatujapata bahati kidogo inayohitajika.”

Huku mashabiki wa timu hiyo wakifurika uwanjani kwenda kuisapoti timu yao, na akaongezea kwa kusema kuwa mashabiki wao wanastahili zaidi. Kosa ni la timu nzima na sii mechi hiyo tuu ambayo bali hata zilizopita hawakufanya vizuri na ni aibu kwamba hawawezi kuendelea kwenye Ligi ya Mabingwa .

Oblak Awaomba Radhi Mashabiki Zao kwa Kushindwa Kufuzu 16 Bora

Wakati huo huo, kocha wa timu hiyo Simeone amehisi kuwa Atletico wametolewa kwenye Ligi ya Mabingwa kwa kukosa penati ya jana ambayo mchezaji wake Carrasco alikosa, huku akitaka mwitikio mkubwa kutoka kwa wachezaji baada ya kutosonga mbele kwenye michuano hiyo.

Simeone amekiri kuwa ni wazi kwamba wangeweza kufunga mabao zaidi kwenye mchezo wa jana lakini kitendo cha jana cha kukosa penati ni kwamba hawatafuti visingizio na si rahisi kupata pointi kwenye mechi ya mwisho dhidi ya Porto ambapo watakuwa ugenini.

Oblak Awaomba Radhi Mashabiki Zao kwa Kushindwa Kufuzu 16 Bora

Oblak na wenzake kwenye michezo mitano ambayo wamecheza ya Ligi ya Mabingwa wameshinda mchezo mmoja, wametoa sare mbili na wamepoteza michezo miwili wakiwa na pointi 5 pekee.

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa