Winga wa klabu ya Chelsea aliyeenda kwa mkpo klabu ya Bayern Liverkusen Callum Hudson Odoi imethibitika hatarudi klabuni hapo katika dirisha dogo la mwezi Januari.

Mchezaji huyo ambaye amekua na kiwango kizuri katika klabu ya Bayern Liverkusen ambapo alitolewa kwa mkopo na klabu yake ya Chelsea kwenda klabu hiyo ya Ujerumani kwa mkopo wa msimu mzima.odoiKuna taarifa zimekua zikiendelea kua mchezaji Callum Hudson Odoi anaweza kurejea katika klabu hiyo ya Chelsea katika majira ya baridi mwezi Januari, Lakini mkurugenzi wa klabu ya Bayern Liverkusen amekanusha taarifa hizo na kusema wanafurahia uwepo wa mchezaji huyo klabuni hapo.

Klabu ya Chelsea imeanza msimu wake mpya wa ligi kuu ya Uingereza vibaya kwani imekua ikidondosha alama mara kadhaa na wachezaji wake muhimu kupata majeraha, Hivo kuwafanya klabu ya Chelsea kufikiria kumrudisha mchezaji huyo.odoiWinga Callum Hudson Odoi ambaye amekua hana wakati mzuri katika klabu ya Chelsea tangu apandishwe kwenye kikosi cha kwanza akitokea akademi ya klabu hiyo, Imeonekana ameafanya vizuri zaidi katika klabu ya Bayern Liverkusen alipo kwa mkopo wa msimu mzima na kuwavutia zaidi mabosi wa Chelsea na kutaka kumrudisha mapema klabuni hapo.

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa