Mnigeria anayekipiga katika klabu ya Fulham iliyoshiriki EPL msimu wa 2020/2021, Ola Aina amefanikiwa kushinda goli bora la msimu kwa klabu yake baada ya kuwapiku wenzake Lemina na Lookman.

Goli alilofunga Aina wakati wa mechi kati yao na West Bromwich Albion limetangazwa kama goli bora la msimu huu wa 2020/2021.

Mchezaji huyo anayecheza kama winga wa Fulham amewashinda wapinzani wake Mario Lemina na Ademola Lookman ambao alikuwa akishindana nao kwenye tuzo hiyo iliyoamuliwa na mashabiki wa Fulham.

Goli hilo hilo la Aina pia liliingia miongoni mwa magoli 10 bora ya msimu huku ile ya tuzo ya goli bora la msimu ikienda kwa Eric Lamela.

Baada ya kutangazwa mshindi wa tuzo hiyo, Ola aliwashukuru mashabiki wa Fulham kwa kumpiga kura na kumuamini kipindi chote alichokuwa uwanjani.

Licha ya kushuka daraja Aina alidai kufurahia kila dakika aliyocheza akiwa na Fulham ambapo alikuwa kwa mkopo kwa mwaka mmoja akitokea klabu inayoshiriki ligi daraja la pili ya Italia.


WEKA PESA KUPITIA DUKANI MERIDIANBET!

Chukua namba yako ya akaunti na kiasi cha pesa unachotaka kuweka, sogea kwenye duka lolote la Meridianbet lililo karibu nawe utasaidiwa kuweka pesa.

Weka Pesa Meridianbet

WEKA PESA

ONI MOJA

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa