Klabu ya Manchester United, ni moja ya klabu ambazo zimekuwa na historia nzuri na ya kuheshimika katika historia ya soka katika Ligi Kuu ya Uingereza na Ulaya kwa ujumla. Ole Gunnar Solskjaer ameaminiwa na klabu ya Manchester United kufanya mabadiliko United, lakini ni kama Man United wameanza kuona kama yupo Masihi wa kuiokoa timu yao na sio Ole Gunnar kwa sasa. Ni vyema angepewa mda zaidi.
Baada ya kutimuliwa Mourinho, Ole Gunnar alianza vyema kabisa kibarua chake akifanikiwa kushinda mechi 14 kati ya 17 za mwanzo akiwa kama meneja, Hata hivyo baada ya kupewa mkataba wa kudumu rekodi inaonesha klabu ya Man United imezidi kudorora katila matokeo yake inayoyapata kwenye michezo mbalimbali.
Mpango wa klabu ulikuwa kumtumia meneja huyu kufanya mabadiliko kwa kipindi cha miaka mitatu, licha ya matokeo ya klabu hii kutoridhisha baadhi ya wadau wanaamini kuwa inahitajika mda wa kutosha ili kuweza kuirejesha klabu kwenye mstari.
United wanamkaribisha Arsenal Jumatatu huku wakiwa na matarajio ya kurekebisha mapungufu ya mechi iliyopita ya EPL dhidi ya West Ham waliyopigwa goli 2:0. Bila shaka watatumia nafasi hii kurejea kwenye nafasi nzuri.
Baadhi ya mashabiki wanafikiri tayari Ole Gunnar tayari ameshindwa kuisimamia klabu hiyo na hivyo labda angetimuliwa tu, hata hivyo kama hili likifanyika kubadilisha mameneja inakuwa ni kama kasumba mbaya huku matokeo yakishindwa kuonekana.
Baadhi ya wataalamu wanasema inahitajika muda wa kutosha kwa meneja kuwepo klabuni na kuzoeana na wachezaji na kufahamu vyema mifumo iunayoweza kufanya kazi katika klabu, pia kugundua aina ya wachezaji klabu inaowahitaji kupambana kwa kiwango kinachohitajika sambamba na kasi ya wapinzani.
Franky
Aondeke uyooo muda wa nn sasa