Ligi ya Kuu Uingereza imeendelea kunoga huku mabingwa wa Ligi msimu uliopita wakilazwa chali kwa mvua ya magoli dhidi ya Aston Villa wikiendi. Manchester United naye alikalia kuti kavu kwa kuruhusu kichapo cha Spurs.
Wikiendi hii ulikuwa ni wakati wa Mourinho kulipa kisasi kwa klabu yake iliyomtimua kazi akiwatandika bao 2-6, kipigo ambacho hakikutarajiwa kabisa kwa Man United kupigwa wakiwa nyumbani.
Mechi iliyoshitua zaidi wapenzi wa soka, na ambayo inaweza kuwa imechana majamvi ya watafutaji makini wa mkwanja kwa kubashiri ni mechi dhidi ya Liverpool. Hakuna aliyetarajia mabingwa kuchapwa 2-7 kama walikuwa wamesimama uwanjani.
Safari ya kipigo ya Man United imeanza dakika ya 4 ya mchezo baada ya Tanguy Ndombele kusawazisha goli la penati lililofungwa na Bruno Fernandes dakika ya pili. Kisha Heung-Min Son akafunga magoli 2, Harry Kane 2, Serge Aurier 1. Anthony Martial alipata kadi nyekundu dakika ya 28. Kipindi cha kwanza kiliwaacha Man U na deni la magoli matatu zaidi, na wakashindwa kufurukuta kipindi cha pili na kumaliza kwa kichapo cha 2-6.
Kwa upande wa Liverpool, wao walianza kuchezea kichapo dakika ya 4 pia, wakifungwa goli lao la kwanza. Kipindi cha kwanza kimeisha Liverpool wakiwa wamechapwa bao 4-1, kipindi cha pili waliambulia goli 1 jingine na kuruhusu Villa kuwapa burudani ya goli 3 zingine. Wikiendi imeisha vibaya kwa mabingwa hawa.
Matokeo ya Jumla Ligi Kuu Wikiendi
Oktoba 3, 2020

Oktoba 4, 2020

Sasa unaweza kuweka pesa moja kwa moja kwenye akunti yako ya Meridianbet kwa kutumia mtandao wa Airtel. Usipate wasi wasi, tunaifanya kazi kuwa rahisi zaidi!


Aziza mushi
Asanteni kwa taarifaa meridianbet.
Janeflora malisa
Asnt kwa taarif
Ester jackson
Liverpool walijiamini sana wakaona wanacheza na timu ambayo ilikuwa hatarini kushuka daraja na kusahau kuwa mchezo unaweza kubadilika mda wowote ule dimbani poleni sana man u na Liverpool mana wote mko sawa
felister
🤣🤣🤣 lakini naogopa
Dorophina
Hakuna wa afadhari wote wamepata kichapo cha mbwa koko
Lydia Emmanuel Magoti
Hamna kitu hapo
magdalena
hakuna ata mwenye nafuu maana wote walichezea kichapo cha aibu sana
Zeiyana
Mourihno kaokota dodo kwenye muarobaini kwanza man u haina kikosi kizuri alafu mourihno kashaitumikia sana ile clabu so haikua kazi ngumu sana kwake..!kwa upanda wa Liverpool naona hunafika mwisho wa klopp kusepa siku zote kutesa kwa zamu zamu yao hishakwisha Liverpool
Fatina mfigi
Mmmh hakuna maan wote alikula kichapo cha mbwa koko!
Angelina
Hamna jambo hapo
Rose kapinga
Wapo hoi hawana jipya wajipange tuu!!!
Adelta
Pole yao
Sadick
Ilikuwa weekend ya matokeo ya kushangaza kweli kweli#meridianbettz
Mwajumah
Hamna kitu apo
Shani
Kloop alidunda vibaya
Hopemwaikuka
Klopp kalala doloooo
Hidaya
Walijisahau sana
Issa
Dah villa on fire pengo la mane linaonekana waz liverpool
Amiri Kayera
Vipgo vya fedhea sana
aisha
Kloop mtu mbaya sijui ka kwama wapi
Sabrina
Aibu babu 😂
Povel
Weekend ya kibabe sana hiii
Tahiya
Ilikuwa no kuchekana na vibes kama lote
Saupha mohamed
Ilikua ya motooo
Sauda
Wote wameambulia kichapo
David Pere
Liverpool walijiamini sana wakaona wanacheza na timu ambayo ilikuwa hatarini kushuka daraja na kusahau kuwa mchezo unaweza kubadilika mda wowote ule dimbani poleni sana man u na Liverpool mana wote mko sawa
Tatu
Kichapo cha klopp kilikuwa cha mbwa koko
Samiah
Duuh
farida ahmadi
Du nouma Sana
Rehema
Watoto wadogowamewatoa jasho
Gabriel
Awachekan wote