Ole Gunnar Solskjaer Ahusishwa Kurejea United

Kocha wa zamani wa klabu ya Manchester United Ole Gunnar Solskjaer anahusishwa kurejea ndani ya klabu hiyo kama mambo yataendelea kua mabaya ndani ya klabu hiyo chini ya kocha Erik Ten Hag.

Ole Gunnar Solskjaer ambaye amewahi kuitumikia klabu hiyo kama mchezaji pia anapewa nafasi kubwa zaidi ya kurejea klabuni hapo kama kocha wa muda endapo klabu hiyo itaamua kuachana kocha wake wasasa.ole gunnar solskjaerManchester United imekua kwenye kipindi kibaya zaidi kwasasa kwenye historia ya klabu hiyo, Kwani mpaka sasa wameshapokea vipigo nane kwenye michuano yote waliyoshiriki msimu huu.

Uongozi wa Manchester United inaelezwa unafatilia kwa karibu mwenendo wa klabu hiyo na matokeo wanayoyapata, Huku wakifikiria kuachana na kocha Erik Ten Hag kama mambo yataendelea kua mabaya zaidi siku za mbeleni.ole gunnar solskjaerKocha Ole Gunnar Solskjaer alifukuzwa klabuni hapo mwaka 2021 baada ya matokeo kua mabaya na klabu kuamua kumfuta kazi, Lakini inaelezwa kuna uwezekano akapewa timu hiyo kama kocha wa muda mpaka mwisho wa msimu kama wataamua kumtimua Ten Hag.

Acha ujumbe