Meneja wa Manchester United Ole Gunnar Solskjaer, anaamini kuwa Walistahili Ushindi kulingana na jitihada za kikosi chake lenye mechi ya Ligi ya Mabingwa Ulaya waliyoibuka na ushindi wa bao 4-1 dhidi ya Istanbul.

Hata hivyo, kwa Ole Gunnar hachululii poa suala la kufuzu kuendelea na hatua inayofuata ya Ligi ya Mabingwa. Anaamini kundi bado liko wazi sana na wanayo nafasi kubwa ya kupenya.
Novemba ilianza kwa mshituko kidogo baada ya Mabingwa hawa kuanza kwa kupoteza mechi yao dhidi ya mabingwa wa Uturuki, na hii ilihatarisha nafasi yao ya kuendelea zaidi hatua ya makundi.

United walirejea na kuwaandikia PSG na RB Leipzig kurejesha tumaini lao la kufuzu hatua inayofuata ya michuano. Hata hivyo, ushindi wa Jana umewasogeza karibu zaidi na mstari wanaohitaji kuvuka kujihakikishia kusonga mbele.

Kwa sasa wanahitaji angalau pointi moja tu kwa kila mechi kwenye mechi 2 zilizosalia.
Kibarua kinachofuata ni dhidi ya PSG, na matumaini yao ni kuwa watapata pointi zote wanaohitaji kusonga mbele kwenye mechi dhidi ya PSG.

Akizungumzia jitihada za Man United kwenye mechi dhidi ya Istanbul Ole Gunnar amesema;

“Kwa kweli nafikiri timu nzima ilicheza vizuri. Tulipata nafasi zetu na umiliki wa mpira, ilikuwa safi sana.

“Tulistahili ushindi, kwa kweli, baada ya kipindi cha kwanza. Nusu ya pili daima ni tofauti na ni ngumu zaidi kulinda ushindi wakati unaposhinda 3-0.”

United wanatoboa hatua ya makundi kwenda kwenye hatua ya mtoano wa timu 16? Tupia maoni yako hapo.


 

USICHELEWE KUKAMATA MKWANJA HUU!

Hadi 130,000,000 TSH Kutolewa kwa washiriki wa shindano la Playson Cashfall. Unaipata kwenye Kasino ya Mtandaoni ya Meridianbet Pekee. Jisajili sasa, kisha ingia mchezoni kabla ya Novemba 29.

Meridianbet Tanzania Casino

SOMA ZAIDI

22 MAONI

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa