Olise Na Msimu wa Kihistoria Uliovunja Rekodi

Michael Olise ameandika hadithi ambayo wapenzi wa soka wataisimulia kwa miaka mingi. Msimu huu tu, amefanya kitu ambacho hakuna mchezaji mwingine amewahi kukikaribia katika historia ya mchezo, kuwa kinara wa asisti kwenye Bundesliga, UEFA Champions League, na Kombe la Dunia kwa wakati mmoja. Huu si msimu tu, ni tamko la ubora, kipaji na ukomavu wa kipekee.

Olise Na Msimu wa Kihistoria Uliovunja Rekodi

Katika Bundesliga, Olise aligeuka injini ya mabao. Kila mechi alionekana kama msanii anayechora pasi za kupasua ukuta wa mabeki. Mashabiki wa soka na ligi hiyo walimfuatilia kama vile unavyofuatilia msanii anayetoa ngoma mpya kila wiki, kila pasi yake ilikuwa hit. Kutawala ligi kubwa kama Bundesliga si jambo dogo, lakini Olise alifanya ionekane rahisi.

Kisha akahamia Champions League, ambako presha huwa juu kwelikweli. Hapo ndipo mastaa wengi hupimwa uzito wao halisi. Lakini Olise hakutetereka. Aliendelea kutoa asisti kwa kiwango cha juu, akiwapa mashabiki wa Ulaya sababu ya kumchora kwenye vichwa vyao kama mmoja wa viungo wabunifu zaidi wa kizazi hiki. Kutawala mashindano haya mawili tayari ni historia, lakini Olise hakusimama hapo.

Olise Na Msimu wa Kihistoria Uliovunja Rekodi

Bila kusahau meridianbet ndio wakali wa ODDS KUBWA, Machaguo zaidi ya 1000 na kila kitu ukitakacho. Bashiri kijanja hapa

Kombe la Dunia ndilo jukwaa la mwisho la kuthibitisha ubora. Wachezaji wakubwa hupimwa hapa. Na Olise, bila kusita, akawa kinara wa asisti duniani. Mashabiki wa soka walipagawa, kuona mchezaji mmoja akifanya maajabu kwenye Bundesliga, Champions League na World Cup ndani ya msimu mmoja ni kama kuona superhero akibadilisha sura tatu tofauti lakini akibaki na nguvu zilezile.

Olise Na Msimu wa Kihistoria Uliovunja Rekodi

Kana kwamba haitoshi, alifunga mabao 30 katika mashindano yote msimu huu. Hii ni namba ya mshambuliaji hatari, si kiungo wa ubunifu. Ndiyo maana msimu wake umeitwa na wengi msimu wa ndoto, na kwa vijana wanaopenda soka la kasi, ubunifu na ujasiri, Olise amekuwa mfano mpya wa kuigwa.

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.