Mshambuliaji wa AC Milan Olivier Giroud anaripotiwa kukataa ofa kutoka kwa vilabu vingi, wakiwemo Manchester City na Tottenham Hotspur ili kusaini Milan msimu uliopita wa joto.
Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 35 aliondoka Chelsea mwishoni mwa msimu wa 2020-21 baada ya miaka mitatu na nusu huko Stamford Bridge, hadi sasa amefunga mabao 11 katika mechi 27 za Milan kwa msimu wake wa kwanza.

Giroud aliripotiwa kuwa mchezaji aliyevutia sana sokoni kabla ya kusaini mkataba wa miaka miwili na kikosi cha Stefano Pioli, huku wakala Vincenzo Morabito amedai kuwa mchezaji huyo wa zamani wa Arsenal alikuwa na mazungumzo na ‘Big Six’ wawili wa Premier League mwaka 2021.
“Alikuwa amechagua kujiunga na Milan tangu Februari, lakini Chelsea ilivunja ahadi ya kumuuza bila ada ya uhamisho. Maldini alimtaka na alikuwa na nia ya dhati ya kumsajili, na Oliver alikubali kupunguzwa mshahara wake ili kusaini Milan” – Morabito
“Inter ilikuwa imemsajili miaka miwili iliyopita. Pia alikuwa hatua moja mbali na Lazio na Juventus. Serie A ilikuwa katika hatima yake huhu ndoa na Milan ikikamilika. Anaweza kuwa mwana Scudetto.”
“Alikataa ofa nyingi ili kusajiliwa na Milan msimu uliopita wa joto. Manchester City, Tottenham, West Ham na New York City walimtaka Olivier, lakini alikuwa amechagua kujiunga na Milan. Sasa ana ndoto ya kushinda Scudetto.”
“Katika majira ya kiangazi Giroud alitaka sana jezi nambari 9 pale Milan. Maldini hakuwa na uhakika kwa sababu ilikuwa imekwenda vibaya kwa wengine, lakini Olivier alivunja laana hiyo na utu wake. Giroud anataka kukaa Rossoneri kwa muda mrefu na kumalizia kazi yake huko Milan.”
Mabao manane kati ya 11 ya Giroud aliifungia Milan yamepatikana kwenye Serie A, na mchezaji huyo wa kimataifa wa Ufaransa hapo awali alifunga bao 90 katika mechi 255 za Premier League alipokuwa na Arsenal na Chelsea.
Mchongo mpya mjini ni Shindano la Evoplay Spring Aweking katika kasino maridhawa za meridianbettz. Pata mgao wako wa TSh 25,000,000 katika michezo kibao ya kasino na sloti ziliyochaguliwa kushiriki.
SOMA ZAIDI HAPA



