Mkuregenzi wa klabu ya Bayern Munich Oliver Kahn ameweka wazi kuwa klabu hiyo ilifanya majadiliano kuhusu kumsajiri mshambulia wa kimataifa wa Ureno anayeichezea klabu ya Man Utd Cristiano Ronaldo ikiwa atafit kwenye mfumo wa timu hiyo.

Cristiano Ronaldo aliandika barua ya kuomba kuondoka kwenye klabu hiyo ili aweze kushiriki michuano ya klabu bingwa Ulaya, na vilabu mbalimbali vilihusishwa na kuhitaji huduma yake huku klabu ya Bayern Munich ikiwemo.

Oliver Kahn, Oliver Kahn: Ronaldo Hawezi Fit Kwenye Mfumo Wetu, Meridianbet

“Tulilizungumzia hili swala vinginevyo tusingekuwa tunafanya kazi yetu vizuri. Mimi namchukulia Cristiano Ronaldo moja ya wachezaji bora kuwai kuwepo kwenye hii dunia.

“Lakini tulikubaliana kwamba licha ya kumkubali Ronaldo , asingeweza kuendana na mfumo wetu wa sasa.” Alisema Oliver Kahn

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa