Kipa wa Ajax, Andre Onana amepunguziwa na adhabu na UEFA baada ya kufungiwa mwaka mmoja kutokana na matumizi ya madawa ya kuongeza nguvu ya Furosemide.
Kipa huyo alikata rufaa baada ya kutumia bahati mbaya madawa hayo ambayo mkewe aliyekuwa mjamzito alikuwa akiyatumia bila kujua athari zake.
Kutokana na kufungiwa huko Onana hatafanya mazoezi na klabu yake ya Ajax tangu mwezi February huku akifanya mazoezi na kocha wake binafsi ili kuendelea kuwa vizuri.
Baada ya Onana kukata rufaa CAS ambapo kesi yake ilisikilizwa wiki iliyopita na huku akishuhudia adhabu hiyo ikipunguzwa kwa miezi mitatu.
Klabu ya Arsenal wanategemea kufufua hamu yao ya kutaka kumsajili mchezaji huyo baada ya adhabu yake kupunguzwa. Mwezi januari iliripotiwa klabu hiyo ilifungua mazungumzo na wakala wa mchezaji huyo.
Chukua namba yako ya akaunti na kiasi cha pesa unachotaka kuweka, sogea kwenye duka lolote la Meridianbet lililo karibu nawe utasaidiwa kuweka pesa.
Kama wamempunguzia vizuri sana
Dah pigo