Golikipa wa klabu ya Manchester United Andre Onana raia wa kimataifa wa Cameroon amefanikiwa kuingia kwenye kinyang’anyiro cha kuwnaia tuzo ya golikipa bora wa mwaka wa Fifa.
Orodha ya magolikipa watakaowania tuzo ya golikipa bora wa mwaka wa Fifa imetoka muda mchache uliopita na Andre Onana ni miongoni mwao akiwa na makipa kama Ederson wa Man City, Yassine Bounou aliyekua anakipiga Sevilla, Thibaut Courtois Real Madrid na Andre Ter Stegen Barca.Golikipa huyo raia wa kimataifa wa Cameron anaungana na magolikipa hao wengine kuwania tuzo ya golikipa bora wa mwaka kutokana na kazi kubwa aliyofanya msimu uliomalizika akiwa na klabu ya Inter Milan ya nchini Italia ambapo alifanikiwa kuhakikisha anaifikisha timu hiyo fainali ya ligi ya mabingwa Ulaya.
Golikipa Andre Onana amekua kwenye kiwango bora sana kwa msimu uliomalizika akifanikiwa kama golikipa aliyekua na hati safi nyingi (cleansheets) katika michezo ya ligi ya mabingwa msimu uliomalizika.Golikipa huyo atachuana na magolikipa wengine bora ambao pia walifanya vizuri msimu uliomalizika kama Ederson wa Manchester City ambaye aliisaidia klabu yake kutwaa mataji matatu msimu uliomalizika ambayo ni taji la ligi ya mabingwa ulaya, Fa Cup, na taji la ligi kuu ya Uingereza.