Uwezekano wa Ousmane Dembele kuendelea kuwepo na Barcelona msimu ujao umeongezeka katika wiki za hivi karibuni kwa mujibu wa Diario Sport.

Mwanasoka huyo ameweka wazi kuwa anataka kurejea tena Blaugrana ingawa wawakilishi wake bado hawajafanya mazungumzo na mamlaka muhimu zenye nafasi ya kuzuia mkataba mpya.

Dembele anapenda kufanya kazi na Xavi Hernandez huko Camp Nou na wawakilishi wake wanapata ugumu kupata timu ambayo itakidhi matakwa yake ya kimkataba.

Juventus, ambao walikuwa na nia na saini yake wanatajwa kuwa hawataki kuwachukiza Barcelona, ambao ni washirika wao katika mradi wa Super League.

Chelsea ambayo iko sokoni, pia imepunguza moto kwenye nia ya saini yake. Bayern Munich na Paris Saint-Germain zote zinatajwa kuwa mbali na mpango wa saini yake.

Manchester United wanatajwa kuwa na nia na staa huyu, lakini haifahamiki kama wapo tayari kukidhi mahitaji ya mkataba wake.

Dembele ameonyesha kile alichonacho katika wiki za hivi karibuni, akithibitisha kuwa mchezaji ambaye ana uwezo wa kufanya makubwa. Kwa mfano, dhidi ya Athletic Club, alifunga bao zuri na kutoa pasi mbili za mabao katika ushindi wa 4-0.


KASINO YA MTANDAONI: EMOTICOINS SABABU YA KUVUNA ZAIDI.

Haijawahi kuwa rahisi hivi kwenye safari yako ya kuvuna mkwanja, kasino maridhawa ya meridianbettz inakuletea mchezo wa Emoticoins unaokupa nafasi ya kufanya safari yako kuwa rahisi zaidi. Wakati ni wako nafasi ni yako na Emoticoins.

senegal, Senegal Mabingwa AFCON 2021., Meridianbet

CHEZA HAPA.

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa