Ozil: Tuliharakishwa Kufanya Maamuzi

Nyota wa ArsenalMesut Ozil amerejea tena kwenye vyombo mbalimbali vya habari. Safari hii akiongelea sakata lake la kugoma kupunguziwa mshahara kama sehemu ya kuendana na madhara ya mlipuko wa Corona duniani.

Ikumbukwe vilabu mbalimbali ulimwenguni vilipendekeza wachezaji wake kupunguziwa mishahara ili wawezekukidhi mahitaji ya kifedha za uendeshaji wa timu hizo. Arsenal ni moja ya timu iliyopendekeza na kutekeleza utaratibu huo.

Mengi yalizungumzwa kuhusiana na Ozil kugoma kupunguziwa mshahara wake lakini pia taarifa kutoka kwa Ozil mwenyewe hazikusikika sana.

Ozil amefunguka kuhusu sakata ilo na ameliongelea kwa ufupi sana akijilenga yeye mwenyewe na kile alichodai ni kulazimishwa kwa wachezaji kufanya maamuzi bila kushirikishwa ipasavyo.

Akizungumza na Athletics, Ozil amesema ” Kama wachezaji, tulitaka kuchangia. Lakini tulihitaji taarifa zaidi na tulikuwa na maswali mengi ambayo hayakujibiwa.”

“Ningekuwa tayari kuchukua hisa kubwa na pengine kukatwa mshahara kama ilipaswa kuwa hivyo mpaka pale mpira na hali ya kiuchumi ikiwa sawa. Lakini tulilazimishwa kufikia uamuzi huo  bila ya kuwa na majadiliano thabiti”.

“Kwa yeyote ambaye angekuwa kwenye hali hii, anahaki ya kujua kila kitu, kujua kinachofanyika na ni wapi pesa inakwenda.”

“Hatukupewa taarifa za kutosha, tulielekezwa kufanya maamuzi tu. Ilikuwa ni mapema mno kwa kitu ambacho kilikuwa ni muhimu na chenye msukumo mkubwa”

“Hii haikuwa sawa, hasa kwa wachezaji wadogo, na nilikataa. Nilipata mtoto na ninahudumia familia hapa Uturuki na Ujerumani na kwenye shughuli zangu za misaada. Nina mradi mpya wa kuwasaidia watu wa London, yale ni maamuzi yangu kutoka moyoni, sio kwa ajili ya kufurahisha watu.”

Ozil alitajwa kama mchezaji pekee wa Arsenal aliyekataa kupunguziwa mshahara katika kikosi cha Arsenal. Katika hili, Ozil amesema “watu wanaonifahamu wananijua ni jinsi gani ninamoyo wa kusaidia wengine. Kwa kile ninachokijua. Mwisho wa siku, sio mimi peke yangu niliyekataa , ila ni jina langu pekee ndio lililotajwa.”

“Nafikiri ni kwasababu ni mimi, na watu wamekuwa wakitaka kunichafua kwa miaka miwili sasa. Wakitaka kunifanya nikose furaha, kuwasukuma mashabiki wanione mimi mbaya na kutengeneza picha ambayo sio sahihi.”

Ozil amecheza michezo yote tangu Arteta alipotua kunako Emirate. Lakini, tangu Ligi Kuu Uingereza – EPL kurejea, Ozil hajacheza mchezo wowote.

Ozil amesema, ” Labda maamuzi yangu yameleta madhara ndani ya uwanja, mimi sijui. Sitoogopa kusimamia kile ninachokiamini kuwa ni sawa, na kama mnakiona kinachotokea sasa hivi kwenye ajira, pengine nilikuwa sahihi.”

Wiki iliyopita, Arsenal walitangaza azimio la kupunguza wafanyakazi 55 na inasemekana wachezaji wamekasirishwa na azimio hilo.


Umekuwa mteja muaminifu wa meridianbet? Basi fahamu kuwa kuna zawadi kibao hadi 5% ya pesa yako inarejeshwa kwako. Kila wiki unaweza kurudishiwa mpaka Tsh 250,000.

Soma zaidi

45 Komentara

    Asante kwa taalifa

    Jibu

    Mmh majanga

    Jibu

    Asante kwa makala

    Jibu

    Ozil muungwana Sana sema vyombo vya habar vinaonekana kutaka kutengeneza clip za kumchafua kwny society

    Jibu

    Nadhani Arteta anatakiwa kumsuka upya Ozil na kujaribu bahati yake, Bado sio mchezaji mbaya sana anaweza kudeliver kitu pale Arsenal kutokana na aina ya uchezaji

    Jibu

    Alicho kiungea Ozil kipo sahii ndio wali taka kumchafua tuu anekane yeye sio mtu kwenye jamii

    Jibu

    Ozil unachosema ni kweli kulingana na maamuzi yako lakini ukumbuke dunia nzima imeyumba kikuchumi sasa sidhani kama ombi lako litawezekana

    Jibu

    Hili Ni bonge la makala
    @meridianbettz

    Jibu

    Maoni:sizani kama ozil anaweza fanya ivyo coz corona imereta athari kubwa sana dunian timu zote ziliyumba kiuchumi

    Jibu

    Histor yake ozil mshahara wake hanagawana na nasikini tumeona afla zake yingi ametoa msaada sahemu yingi na ndio maana naona hataki mshaara wake upunguzwe big up sana maana naji ozil tetea aki yako

    Jibu

    Makala mzuri

    Jibu

    Ukweli humuweka mtu huru sio kama kwetu kati ya viongozi na wachezaji ni ujanja ujanja tu hawaeleweki nani mkweli na nani muongo

    Jibu

    Arteta amfue vizr ozir Kila kitu kutakua sawa

    Jibu

    Duuuh Mambo hayo

    Jibu

    Hatarii

    Jibu

    Arteta ana kazi Sana kwa uyu Ozil

    Jibu

    Hatari sana!!!

    Jibu

    Kumbe Ozil anaijua pesa Kama amezaliwa moshi vile😀

    Jibu

    Duuh Mambo ayo#Meridianbettz

    Jibu

    Uje siku zote pale kunapotokea matatizo lazma ukubaliane nayo Kuna timu nying sana zilifanya mbadala wa kupunguziwa misharaha kutokana na majanga ata baadhi ya makampun yanafanya hivyo ili kufanya kuendeleza makampun yao me naona sio busara kwenda kwenye vyombo vya habar kuongea hivyo maaana unaidharirisha club yako

    Jibu

    Yuko sahihi kabisah ozil

    Jibu

    Duuh poleni sana

    Jibu

    Ozil hayupo sahihi,inajulikana duniani kote kwamba Corona imeathiri uchumi wa kila sekta ikiwa ni pamoja na vilabu vya mpira, alipaswa kuona hilo na kupunguza mshahara wake#meridianbettz

    Jibu

    Duuu hatareee sana

    Jibu

    Hatar sana

    Jibu

    Duh hii corona hii inarudisha watu nyuma

    Jibu

    Du aya majanga

    Jibu

    asnte kwa taarif

    Jibu

    Tatz hil

    Jibu

    Asante kwa taarifa za kimichezo

    Jibu

    duh ilo sasa balaa nalo

    Jibu

    Goodupdate

    Jibu

    Duuh maganga hayooo

    Jibu

    Duuuh

    Jibu

    Asante kwa taarifa

    Jibu

    majanga

    Jibu

    Kwanini jaman!!! Tatizo ilo!!!

    Jibu

    Duuh atarii

    Jibu

    Aisee

    Jibu

    Anazingua ozil

    Jibu

    Ujue siku zote pale kunapotokea matatizo lazma ukubaliane nayo Kuna timu nying sana zilifanya mbadala wa kupunguziwa misharaha kutokana na majanga ata baadhi ya makampun yanafanya hivyo ili kufanya kuendeleza makampun yao me naona sio busara kwenda kwenye vyombo vya habar kuongea hivyo maaana unaidharirisha club paspo sababu

    Jibu

    Namuonaga Ozil Muongo Muongo#Meridianbettz

    Jibu

    Ozil kwa maneno yake anaonekana kuwa anatoa msaada mkubwa sana kwa jamii

    Jibu

    Ozil fundi .

    Jibu

    Wanalipw pesa nyingi lakn Awana utu

    Jibu

Acha ujumbe