Pablo : Mbeya City ni Bora, Tunahitaji Umakini.

 

Klabu ya Simba SC ikiongozwa na kocha Pablo inashuka dimbani katika uwanja wa Sokoine, Mbeya kuvaana na Mbeya City katika mchezo wa Ligi Kuu ya NBC leo saa 10 jioni.

 

Kocha Mkuu wa Simba SC, Pablo Franco, amesema mchezo utakuwa mgumu kutokana na uwezo wa wapinzani ukichangiwa pia na aina ya uwanja ambao watatumia.

“Mchezo utakuwa mgumu, Mbeya City ni timu bora, tunaenda kucheza kwenye uwanja ambao hauta turuhusu kucheza mpira wa chini. Tunahitaji kuwa makini na mipira ya kutengwa ili tuwe salama,” amesema Pablo.

Akizungumza kwa niaba ya wachezaji, Shomari Kapombe amesema wanahitaji kushinda ili kuendeleza walipoishia baada ya kutwaa ubingwa wa Kombe la Mapinduzi Alhamisi iliyopita.

“Tumetoka kushinda Mapinduzi, tunapaswa kushinda tena leo ili kuendeleza morali ya kufanya vizuri kwenye ligi ambayo tumerejea,” amesema Kapombe.


JIACHIE NA ALMIGHTY AZTEC

Ni muda wako kujiachia na mchezo maridhawa wa Almighty Aztec katika kasino bomba za meridianbettz. Nafasi ya kutengeneza mkwanja iko mikononi mwako kazi ni kwako.

tetesi, Tetesi za Soka Barani Ulaya., Meridianbet

CHEZA HAPA

Acha ujumbe