Kwanza baba yake Cesare Maldini, au ukipenda muite Maldini Senior alikuwa mchezaji bora ligi kuu ya Italy miaka ya 60. Nadharia inasema wachezaji bora hawazai wachezaji bora.
Ni wachache sana wamefanikiwa, kama ‘the great Mazinho’ baba mzazi wa Thiago Alcantara na Wael Rafinha. Kesper Schmeichel wa Leicester, mtoto wa Peter Schmeichel. Hapa kwetu kuna kizazi cha Sureboy. Salum Abubakar ni mtoto wa winga wa zamani wa Yanga Afrika, Abubakar Salum.
Basi pale Italy kipo hiki kizazi cha Maldini. Mzee Cesare Maldini, alikuwa beki aliyehudumu AC Milan kwa mafanikio makubwa. Maldini Sr anabaki kuwa muitaliano wa kwanza kunyanyua klabu bingwa Ulaya kama nahodha. Amecheza mechi ya zaidi ya 300 pale AC Milan.
Miaka 20 baada ya mzee Cesare kutupa taulo ulingoni, kijana wake Paolo alicheza mchezo wake wa Kwanza. Huyu Paolo hakuwahi kumuona baba yake akicheza. Kwanza alizaliwa wakati baba ameshastaafu.
Akianza kama beki wa kulia baadae alihamia kushoto na hapo ndipo dunia ililifahamu jina lake vema. Kumbuka mguu wake wa asili ni kulia, lakini aliweza kutumia mguu wa kushoto kuliko namna ambavo wachezaji wengi tu waliweza kuitumia miguu yao ya asili.
Siku anaingia uwanjani kucheza mchezo wake wa kwanza alikuwa na miaka 16 tu, baada ya hapo lilifuata lile neno la siku zote, ‘kilichofuata ni historia tu”. Aliichezea AC Milan mechi zaidi ya 900 kwa miaka 25 aliyodumu pale, ameshinda kila kitu pale Milan.
Alijitoa kwa ajili ya AC Milan, katika maisha yake yote kichwa chake kilijua kitu kimoja tu, kuwa yeye ni mchezaji wa AC Milan. Mwaka fulani sir Alex Ferguson alijaribu kumsajili kupitia baba yake.
Cesare Maldini hakuwa na maelezo mengi kwa Sir Alex Ferguson, alimuambia “My grandfather was Milan, my father is Milan, I’m Milan and my son is Milan. Forget it.”
Naam, baba alikuwa anamuhakikishia kuwa, damu yao ni AC Milan na hawawezi kubadilika kamwe.
BONASI YA 50% KILA SIKU KATIKA KASINO ZA EVOPLAY HAPA MERIDIANBET.
Meridianbet na Evoplay Kasino wanakupa bonasi ya 50% ya kiasi utakachoweka katika akaunti yako leo. Unasubiri nini ni wakati wa kupiga pesa sasa na Mabingwa.
Safi sana