Hadi sasa uongozi wa Simba umeingia katika hali ya kigugumizi juu ya uamuzi wao wa kumuuza winga wao Pape Ousmane Sakho au kumbakisha ndani ya timu hiyo wakihofia kuyakuta yale yaliyowatokea kwa wachezaji wao Luis Miquissone na Chama.

Chama na Luis wote waliuzwa katika dirisha kubwa la msimu uliopita jambo ambalo lilipelekea Simba kushindwa kutamba na kujikuta wakishindwa kupata ubingwa wowote msimu uliopita.

Sakho ambaye amefanikiwa kutwaa tuzo ya bao bora la mwaka kutoka kwa shirikisho la soka Afrika CAF,kwa sasa anagombewa na zaidi timu nne kutoka nje ya Tanzania na Afrika zikiwemo Orlando Pirates,Wydad Casablanca na Raja Casablanca zote za Morroco..

Chanzo cha habari ambacho kiliomba hifadhi ya jina kilisema kuwa Uongozi wa Simba upo katika majadiliano ya kuona ni namna gani wataweza kuamua hatma ya Sakho kama wataweza kumuuza au wambakishe kulingan na ofa ambazo zimemiminika ndani ya timu hiyo.

“Viongozi kwa sasa wanajadili kama wamuuze Sakho au wambakize,tayari kuna ofa nyingi kutoka katika timu kubwa za Afrika na nyingine Ulaya,uongozi unaangalia jambo lipi litakuwa sahihi kwao haswa katika maamuzi kama watamuuza.

“Ambacho kinaangaliwa ni je kama wataamua kumuuza Sakho mbadala wake utakuwa ni nani wakati mipango yao ni kufanya vyema tena katika michuano ya kimataifa,jambo hilo ndio linatoa ugumu kwa uongozi wakihofia kuyakutana ya Miquissone na Chama ambao waliondoka kisha Simba ikapata tabu msimu uliopita,” kilisema chanzo hiko.

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa