Paqueta Kubakia Westham

Kiungo wa klabu ya Westham United Lucas Paqueta imethibitika atabakia ndani ya klabu hiyo baada ya uongozi wa Manchester City kupiga chini dili hilo.

Manchester City walikua wanamuhitaji kiungo Paqueta kwajili ya kuongeza nguvu kwenye kikosi chao msimu huu, Lakini viongozi wa klabu hiyo wamepiga chini suala kumsajili mchezaji kutokana na kiwango cha pesa kilichowekwa na klabu ya Westham.paquetaManchester City kwasasa wanataarifiwa kuangalia uwezekano wa kutafuta mchezaji mwingine katika nafasi ya kiungo, Hiyo ikitokana na kupiga chini dili la kiungo huyo wa kimataifa wa Brazil na ikitokana na kushindwa kufika bei yake.

Kocha wa Manchester City alieleza wazi siku kadhaa nyuma watakwenda kwa wachezaji ambao wataweza kuwasajili kutokana na kiwango chao cha pesa na kusema wachezaji ambao bei zao ni kubwa na hawawezani nao bei zao hawatawasajili.paquetaKiungo Lucas Paqueta amekua kwenye ubora mkubwa ndani ya klabu ya Westham tangu ajiunge nao msimu uliomalizika akitokea Olympique Lyon na yeye alikua tayari kujiunga na City, Lakini bei waliyoweka Westham iliwafanya City kusitisha mpango wa kumnunua.

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.