Klabu ya Juventus imetoa tamko kuthibitisha kuwa Fabio Paratici amepewa taarifa juu ya haki ya kujitetea juu ya Kesi ya Luiz Suarez.

Ofisi ya Mwendesha Mashtaka kwenye Korti ya Perugia wamefanya uchunguzi juu ya ofa ya nyota huyo wa Atletico Madrid kuhamia Juventus, wakati Suarez akikamilisha masharti ya kupata uraia ili kuepuka msharti ya sheria ya kawaida ambayo hutumika (Non-EU Rule).

Kufanyika kwa mchakatowa kupata uraia wa staa huyu ambao unahofiwa kuwa ulikuwa ni ukiritimba wa kukiuka taratibu umepelekea uchunguzi ambao unaendelea sasa kwa mameneja wa Juventus.

Katika taarifa yake, Juventus wametaja kuwa meneja Fabio Paratici amefahamishwa juu ya haki yake ya smingi na lazima ya kujitetea.

Hata hivyo, klabu inaamini kuwa kuna kutoelewana mahali juu ya suala hili, na kwao wanaamini kuwa ni suala la muda kabla ya matokeo ya uchunguzi kubainisha nafasi ya meneja wao kuwa hakukuwa na ukiukaji wa sheria.


 

FURAHIA MUZIKI MTANDAONI HUKU UKITENGEZA MKWANJA!!

Mchezo wa Astro Legend unakupatia burudani ya muziki kupitia kasino ya mtandaoni ya Meridianbet. Utaburudika huku ukiendelea kutengeza mkwanja mrefu, jiunge sasa na uwe miongoni mwa mabingwa!!

Paratici, Paratici Kuchunguzwa Kesi ya Suarez, Meridianbet

INGIA MCHEZONI

15 MAONI

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa