Kiungo wa PSG, Leandro Paredes ameweka wazi kuwa Juventus walijaribu kumsajili miaka 9 iliyopita, lakini wakala wake alikataa dili la uhamisho huo.

Kibibi Kizee cha Italia kimekuwa kikihusishwa na staa huyu wa Argentina miezi ya hivi karibuni huku staa huyu mwenye miaka 25 ambaye alisha wachezea Chievo, Roma na Empoli kule Italia, amesema kuwa ilibaki kidogo sana kujiunga Juventus alipokuwa bado kinda.

Akizungumza na kituo cha TNT Sport, Paredes anasema Mkurugenzi wa Juventus alijaribu kumnunua mwaka 2011 ili aende kuwa kilaka cha Adrea Pirlo.

Paredes: Juventus Walinihitaji 2011
Leandro Paredes akiwa Empoli 2015/16

Wakala wake aliona kama Juventus walikuwa wamepagawa wakati huo, ambaye alimnukuu kuwa alisema Juventus “Walikuwa machizi” kwa ofa hiyo.

Pareds anasema

“Mwaka 2011, Mkurugenzi wa Juventus alijaribu kuninunua alisema ananihitaji kutoa msaada kwa Pirlo. Wakala wangu alisema walikuwa machizi, nika salia Boca Juniors.”

Kwa mujibu wake Pareds, kipindi alichokitumia kwa mkopo pale Empoli 2015-16 kilimfunza mambo mengi akifanikiwa kuwa kiungo tegemezi wa Marco Giampaolo.

37 MAONI

  1. Wakala wake aliona kama Juventus walikuwa wamepagawa ndo maana akutaka kwenda Juventus pia psg walitoa ofa kubwa kidgo#meridianbettz

  2. Asante kwa habari nzuri Ila mawakala wasiwakwamishe wachezaji katika swala la pesa kwani wakifanya hivyo wanawashusha kimaisha.

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa