Partey Bado Yupo Sana Arsenal

Kiungo wa klabu ya Arsenal na timu ya taifa ya Ghana Thomas Teye Partey amesema anajua taarifa mbalimbali zinazoendelea lakini yeye binafsi ana furaha kuendelea kuwepo ndani ya Arsenal.

Kiungo Partey amekua akihusishwa kuondoka ndani ya klabu ya Arsenal tangu dirisha kubwa la usajili lililopita, Lakinin bado ameendelea kuwepo ndani ya klabu ya Arsenal na ameeleza bado anatamani kuendelea kuwepo klabuni hapo.parteyKiungo huyo ambaye amekua akiandamwa na majeraha mara kwa mara ndani ya kikosi cha Arsenal amezungumza haya baada ya kutoka kwenye majeraha ambayo yalikua yakimsumbua wiki kadhaaa zilizopita.

Vilabu mbalimbali kutoka nchini Saudia Arabia pamoja na ulaya vilielezwa kufukuzia huduma ya kiungo huyo, Lakini klabu ya Arsenal hawakua tayari kumuachia kiungo huyo katika dirisha kubwa lililopita.parteyThomas Partey amekua moja ya wachezaji muhimu ndani ya kikosi cha Arsenal pale ambapo anakua fiti bila majeraha, Lakini mara kadhaa amekua akiandamwa na majeraha jambo linalofanya kuibuka kwa tetesi za yeye kutimka klabuni hapo.

Acha ujumbe