Paul Merson ameamua kutoa ya moyoni kuhusu Mesut Ozil ndani ya kikosi cha Arsenal. Hii ni baada ya mjerumani huyo kutupwa nje ya kikosi cha timu hiyo msimu huu.

Paul Merson anaamini, kama Partey amepatiwa nafasi kwenye kikosi cha Arsenal basi Ozil anapaswa kurudishwa kwenye kikosi hicho.
Paul Merson, Paul Merson “Kama Partey Anacheza, Ozil Anaweza Kucheza”, Meridianbet
Thomas Partey.

Paul Merson ambaye aliwahi kuwa mshambuliaji wa Arsenal amenukuliwa akisema “Kwa upande wangu, Ozil anawezakupewa nafasi kwenye kikosi kama Partey anacheza vizuri.

Partey anatawala safu ya kiungo na mchezo kwa ujumla. Anavyocheza Partey, anafungua nafasi kwa Ozil. Kwa sasa, Arsenal hawana mtu wa kuwalisha washambuliaji. Utakimbia uwanja mzima, lakini ukiwa kama mshambuliaji , mbio zako zitazaa matunda kama utakuwa na mchezaji mwenye mbio kama zako nyuma yako.”

Paul Merson, Paul Merson “Kama Partey Anacheza, Ozil Anaweza Kucheza”, Meridianbet
Mesut Ozil Akiangalia Moja ya Mechi za Arsenal.

Arsenal wanataabika msimu huu wakiwa wanashika nafasi ya 14 kwenye msimamo wa EPL wakiwa na ushindi wa mechi 1 kati ya 6 walizocheza kwa siku za karibuni. Hii ni kusema kuwa Mesut Ozil amelaani maamuzi ya Arteta au Arsenal wanakwama wapi??


FURAHIA MUZIKI MTANDAONI HUKU UKITENGEZA MKWANJA!!

Mchezo wa Astro Legend unakupatia burudani ya muziki kupitia kasino ya mtandaoni ya Meridianbet. Utaburudika huku ukiendelea kutengeza mkwanja mrefu, jiunge sasa na uwe miongoni mwa mabingwa!!

Paul Merson, Paul Merson “Kama Partey Anacheza, Ozil Anaweza Kucheza”, Meridianbet

INGIA MCHEZONI

22 MAONI

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa