Paul Pogba, Hakuna Jipya.

Wakati Manchester United wakiwa wamebakiza michezo 10 tu kuhitimisha msimu wa 2021/22 kwenye EPL, hakuna jipya kuhusu mkataba wa Paul Pogba.

Pogba anaelekea kumaliza mkataba wake wa miaka 5 na Man United (mwishoni mwa msimu huu) na, kwa hali ilivyo, hakuna maongezi ya mkataba mpya toka mwezi Julai mwaka jana.

Inaripotiwa kuwa, uongozi wa United ulimpatia ofa ya mkataba mpya lakini, Paul Pogba na wakala wake, hawakujibu chochote kuhusu ofa hiyo. Hii ni hali inayozua sintofahamu kuhusu mchezaji huyo ambaye pia, anahusishwa na PSG na Real Madrid.

Japokuwa haijafahamika wazi kama lengo la Pogba ni kuondoka kama mchezaji huru au anachagiza maboresho zaidi kwenye mkataba aliopewa au lengo lake hasa ni lipi? Yote kwa yote, United inakazi kubwa ya kufanya katika maboresho ya kikosi mwishoni mwa msimu huu.

Kumpata kocha mpya wa muda mrefu, kuuza baadhi ya wachezaji, kununua wachezaji wapya, kuboresha mifumo ya uongozi wa klabu chini ya uongozi wa Mkurugenzi mpya n.k ndio vipaumbele kulekea majira ya joto.


VUNA MKWANJA NA SHINDANO LA EVOPLAY SPRING AWEKING

Mchongo mpya mjini ni Shindano la Evoplay Spring Aweking katika kasino maridhawa za meridianbettz. Pata mgao wako wa TSh 25,000,000  katika michezo kibao ya kasino na sloti ziliyochaguliwa kushiriki.

tetesi, Tetesi za Soka Barani Ulaya., Meridianbet

SOMA ZAIDI HAPA

Acha ujumbe