Paul Pogba na Ufalme Usiotimilika Pale Old Trafford

Ni ngumu kumchukia yule unayempenda, hata akikupa sababu za kumchukia bado utaendelea kumpenda maana upendo hudumu na kuvumilia yote. Paul Labile Pogba katika kichwa chake ana ramani nzima ya Manchester united namna inavyotakiwa kucheza kwa sasa, ni siri ambayo inaishi katika kichwa chake, utaiona pale tu miguu yake ikiwa inakanyaga nyasi za Old Trafford.

Katika dimba la kati la Manchester united anaichora mipango yote ya mashambulizi ya timu, kuna tofauti kubwa sana ya Manchester united ikiwa na Pogba uwanjani na ile ambayo haina Pogba uwanjani.

Yenye Pogba uwanjani inachangamka sana katikati, timu inapanda kupitia miguu ya Pogba, ni rahisi kumwona mshambuliaji Anthony Martial akiokota mpira baada ya kufunga goli tamu lenye pasi ya miguu ya Pogba.

Ana umuhimu mkubwa uwanjani, Manchester United isipokuwa na Pogba uwanjani kuna ufundi unapungua wanapata shida sana kushinda.

Uzuri wa pogba ana uwezo wa kucheza maeneo muhimu yote ya kiungo itategemea kocha anamtaka kwa matumizi yapi, akicheza kama kiungo mchezeshaji ni kama vile unakitazama kiuno cha shakira katika vazi lake laini.

Anasukuma mipira mbele kwa kasi ya ajabu, akicheza kama kiungo mshambuliaji ni kama kumpa mchawi mtoto akulele, Pogba hapa anapiga mashuti golini kisha anatoa assist kizuri zaidi anakupa na kufunga pia.

Yote haya yanapatikana katika kichwa chake, mashabiki wanalitambua hilo, licha ya mambo yote aliyoyafanya bado wamefunga macho na mdomo wakiamini wanamhitaji zaidi kuliko anavyowahitaji.

Alitamka wazi anataka kuondoka Manchester United, bodi ya timu wakaweka pamba masikioni naamini hawakusikia hilo. Kwa sasa jina lake na Bruno Fernandes ndiyo habari ya mjini kila mtu anazungumzia kuhusu hilo, wamepata sababu ya kumpenda tena, ndivyo maisha yalivyo.

Paul Pogba anabakia kuwa mchezaji mzuri ambaye kila timu inatamani kuwa naye, siwashangai Manchester united kuamua kufunga macho katika hili.

45 Komentara

    Huyu jamaa sija wahi kumuelewa kabisa yani#meridianbet

    Jibu

    Baada ya kuanza kazi yake na Manchester United mwaka 2011, Pogba alijiunga na timu ya Italia Juventus mwaka 2012, na akisaidia klabu hiyo kwa mataji manne ya Serie A, pamoja na Coppa Italia mbili na mataji mawili ya Supercoppa Italiano. Wakati akiwa na klabu, alitambulisha kama mchezaji mdogo sana duniani, na alipokea tuzo ya mchezaji chipukizi mwaka 2013, ikifuatiwa na Tuzo ya Bravo mwaka 2014 na aliitwa na The Guardian kama mmoja kati ya wachezaji kumi vijana wa Ulaya. Mwaka wa 2016, Pogba aliitwa mchezaji bora wa ya UEFA mwaka 2015 na kupewa zawadi na FIFA FIFpro, baada ya kusaidia timu yake ya Juventus hadi mwisho wa Ligi ya Mabingwa wa UEFA 2015.pia Pamoja na kuondoka Manchester United kwa uhamisho wa bure, Pogba alirudi klabu mwaka 2016 kwa ada ya kubwa zaidi ya uhamisho na kuwa kumbukumbu ya dunia ada ilikuwa ni € 105 milioni (£ 89.3 milioni).
    Ndani ya taifa lake alikuwa chini ya kiwango cha- 20,aliipatia taifa lake ushindiwa kombe la mataifa ya ulaya la FIFA U-20 ndani ya mwaka 2013 na alichukua tuzo ya mchezaji bora kwa maonyesho yake wakati wa mashindano hayo. Alifanya timu yake ya ya taifa ya ufaransa kupata ushindi wa 3-1 dhidi ya Georgia tarehe 22 Machi 2013, na alifunga bao lake la kwanza la Kombe la Dunia mnamo Juni 30, 2014 dhidi ya Nigeria; alipewa tuzo ya mchezaji bora kijana kwa mbwembwe zake katika Kombe la Dunia la FIFA ndani ya mwaka 2014, baada ya kufikia robo ya mwisho. Baadaye aliwakilisha taifa lake katika UEFA Euro 2016 kwenye kiwanja cha nyumbani, ambapo alifunga bao moja lililo dumu hadi mwisho wa mchezo

    Jibu

    Pogba inapaswa atulie sababu ni mchezaji anaefit vizuri sehemu ya kiungo hivyo akitulia na akinipa united mataji zaidi ufalme ataufikia tu

    Jibu

    Pogba ni mchezaji mzuri sana anaweza akautimiza ufalme wake akitulia na kuifanya man united kuwa juu na kuchukua vikombe vingi zaidi

    Jibu

    Pogba ni mchezaji mzuri Sana ila amepata jina kubwa katika career yake ya mpira lakini hadi sasa ajawafanyia wana man u kitu kikubwa.

    Jibu

    Pogba anafanya mambo makubwa sana ,

    Jibu

    Mi simuelewag kabsa

    Jibu

    Pogba mtu mbaya

    Jibu

    Pogba yupo vzr jmn

    Jibu

    Pogba mchezaji mahiri sana

    Jibu

    Kiungo fundi

    Jibu

    Paul ana makosa madogo madogo ambayo yanaweza kurekebishika tu endapo akituliza akili yake

    Jibu

    Mchezaj bola uyu kabx

    Jibu

    Kama sikosei huyu fundi wa ki france paul pogba ni kiungo ghali sana dunian bado ana mapenzi na club ya Manchester United ila mara nyingi wakala ndio ana myumbisha ila kwa sasa naona kabisa moyi wake kwa sasa anataka kucheza wapi anaonekana mtu mwenye furaha akiwa ana drible mpira anavyotoa pasi na kutoa ushirikiano mkubwa na timu kwa ujumla

    Jibu

    Pogba anajua sana anacho kifanya na kina umuhimu gani kwake

    Jibu

    Pogba anafanya Mambo mazuri sana

    Jibu

    Ni mchezaji mzuri

    Jibu

    Pogba ni mchezaji mzuri sema usharobaro ndio unamkosti sana

    Jibu

    Pogba Ni mchezaji mzuri sana na kiungo mzuri sn kwenye gemu

    Jibu

    Hata mie namkubali sana#Meridianbettz

    Jibu

    Pogba ni mchezaji mzuri lkn hakuna chochote cha kumbukumbu alichokifanya man u

    Jibu

    Pogba Ni mchezaji mzuri sana

    Jibu

    Pogba amekuwa ni mtu asioeleweka Nini anafanya

    Jibu

    Ni mchezaji mzuri

    Jibu

    Daah pogba ni mchezaji ninaemkubali sana#Meridianbettz

    Jibu

    Paul pogba ni mchezaji mzuri

    Jibu

    Paul pogba namkubali kinoma unajua Bina damu lazima awe namapungufu akuna mtu asie kuwa na mapungu ndio pogba anamapungufu yake Ila yanafaa kulekebishwa anajua anajituma mpambanaji Hilo mulihelewe

    Jibu

    Pogba anajua sana

    Jibu

    Pogba ni mchezaji mahili sana

    Jibu

    Hakika pogba ni mchezaji mzur kila timu nzur inataman kuwa naye

    Jibu

    Mchezaji mzur sana

    Jibu

    Uzuri wa pogba anaweza kucheza maeneo muhimu

    Jibu

    Paul pogba ukiachana na paul schools na wayne rooney na carrick huyu ndio mchezaji anaetoa assists pale man u na anapiga pass ndefu za kuamisha uwanja kama paul schools na wayne rooney anafanya vizuri sana na combination yake na bruno imekaa sawa sana ndio man u ya sasa ipo moto kila anaekuja anachezea

    Jibu

    Pogba namkubali san#meridianbettz

    Jibu

    Binafsi natamani sana Pogba kusepa Man U sema tu ukata umetawala katuika club nyingi na dau lake kubwa kwenye swala la uhamisho

    Jibu

    Pogba yupo vizuri sana

    Jibu

    Habar njema

    Jibu

    Maoni:Pogba mkali wao

    Jibu

    Hatari sana huyu pobga.

    Jibu

    Pogba yupo vizuri

    Jibu

    Ufalume wake utatimilika Kama ataamua kusaini mkataba mpya na kutuliza akili take pale OT atatimiza malengo yake

    Jibu

    Pogba yupo vizuri

    Jibu

    kiungo fundi

    Jibu

    Pogba man u kwa sasa ndipo panapokufaa tulia upige kazi.

    Jibu

    Ana umuhimu mkubwa uwanjani, Manchester United isipokuwa na Pogba uwanjani kuna ufundi unapungua wanapata shida sana kushinda.

    Jibu

Acha ujumbe