Kiungo wa Manchester United, Paul Pogba yupo njia panda juu ya hatma yake klabuni hapo. Staa huyu ansema kuwa bado hajapewa dili la maana na Man United.

Mkataba wa sasa wa staa huyu unafika tamati Juni mwakani, na akiwa hajapata mkataba mpya kumekuwa na stori nyingi juu ya sintofahamu ya hali yake ya mkataba.

Ripoti za hivi karibuni zilibainisha kuwa Mashetani Wekundu tayari walikuwa wameshaanza mazungumzo na staa huyu kwa nia ya kukubaliana mkataba wake mpya.

Paul Pogba

Hata hivyo, Paul Pogba kwa upande wake amekanusha madai ya kufanya mazungumzo yeyote ya msingi juu ya mkataba wake na Man United, kwa sasa akili yake ameielekeza katika michuano ya Euro 2020 akiwa na timu yake ya taifa ya Ufaransa.

Nina mwaka mmoja umesalia kwenye mkataba wangu na kila mtu anatambua hilo. Hakujawa na mapendekezo yeyote ya msingi ya kuongezwa kwa mkataba. Bado nipo Manchester. Baada ya msimu kulikuwa na likizo, hivyo sikuweza kukaa chini na meneja na kocha. Nimejielekeza kwenye Euro kwa sasa.”

– Paul Pogba

WEKA PESA KUPITIA DUKANI MERIDIANBET!

Chukua namba yako ya akaunti na kiasi cha pesa unachotaka kuweka, sogea kwenye duka lolote la Meridianbet lililo karibu nawe utasaidiwa kuweka pesa.

Weka Pesa Meridianbet

WEKA PESA

 

 

 

ONI MOJA

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa