Paul Scholes kiungo fundi wa zamani wa klabu ya Manchester United na timu ya taifa ya Uingereza ametaja goli lake bora la muda wote wakati akicheza mpira.

Tofauti na ilivyotarajiwa na wengi kiungo huyo alitaja goli lake dhidi ya Aston Villa Disemb 23 kwenye msimu wa 2006/07 katika mchezo walioshinda goli tatu kwa bila huku yeye akifunga goli zuri la kuunganisha baada ya kona nzuri iliyopigwa na Ryang Giggs kuokolewa na mpira kukutana na Scholes nje boksi na kuunganisha mpira vizuri (Volley) na hilo goli analiona kama goli bora zaidi katika maisha yake ya soka.

paul scholesWatu wengi walikua wakidhani labda angetaja goli alilofunga dhidi ya Fc Barcelona katiika nusu fainali ya ligi ya mabingwa ulaya kwenye msimu wa 2007/08 na kuwapeleka United Fainali ya michuano hiyo na mwaka huo klabu hiyo kufanikiwa bingwa wa michuano hiyo,Ila Paul yeye anasema “Nilipiga mpira vibaya lakini linabaki kama goli muhimu zaidi katika maisha yangu ya soka”.

Pia kwenye mahojiano hayo Scholes alimpakulia minyama kiungo mpya wa klabu hiyo Christian Eriksen na kusema “Ni kiungo mwenye maarifa makubwa na anayecheza kwa kutumia ubongo wake zaidi kwasababu anajua anatakiwa kua sehemu gani uwanjani na pia anajua wenzake wapo wapi katika dimba”.

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa