Pedri mchezaji wa klabu ya Fc Barcelona pamoja na timu ya taifa ya Hispania maarufu kama La roja amesema timu ya taifa ya nchi hiyo ni miongoni mwa timu zinazopewa nafasi ya kubeba kombe hilo mwaka huu pale nchini Qatar.

Kikosi hicho kinachonolewa na mwalimu Luis Enrique kocha wa zamani wa klabu ya Barcelona amefanikiwa kuijenga timu hiyo kupitia vijana wadogo wanaofanya vizuri na kuifanya kua timu bora kwa muda wa miaka miwili kitu kinachofabya watu wengi kuwapa nafasi mabingwa hao wa zamani wan kombe la dunia.

pedriTimu hiyo ambayo itaanza michuano hiyo ndani ya miezi miwili mbele dhidi ya Costa Rica na kiungo huyo anaamini kizazi cha kinaweza kufanikisha kubeba kombe la dunia kwa mara ya pili baada ya kubeba la kwanza mwaka 2010.

“Pengine watu watu hawatarajii mengi kutoka kwetu, na labda sisi sio kipaumbele cha watu wengi lakini ndani yetu tunaona tunapendwa”.

“Hatuvaa medali bila kupambana inavyotakiwa na kama tutapambana inavyotakiwa basi tutavaa medali”

“Siku zote kumekua na changamoto kuanzia Barca na timu ya taifa lakini kama mchezaji unatakiwa kua mtulivu na kufurahia tu”

Timu ya taifa ya Hispania imefanya vibaya tangu ibebe kombe hilo mwaka 2010 pale Afrika ya Kusini yamepita mashindano mawili wakiishia hatua za kawaida 2014 wakiishia hatua ya makundi huku 2018 pale Urusi wakiishia hatua ya 16 bora hivo mwaka huu inaweza kua nafasi ya kurudisha ubora wao uliopotea kwenye michuano hiyo baada ya kocha Luis Enrique kutengeneza timu ya ushindani iliojaa vijana wadogo wenye uwezo mkubwa.

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa