Pengo la Hazard Halina Mwenyewe - Drogba

Kwa mujibu wa wa aliyekuwa mshambuliaji wa klabu ya Chelsea, nyota Didier Drogba, pengo la Eden Hazard klabuni Cheslea halina mchezaji anayeweza kuliziba kwa sasa. Drogba anaamini Hazard atakumbukwa kama shujaa klabuni hapo.

Hazard alisepa klabuni hapo mwezi Juni 2019 akienda kutimiza ndoto yake ya tangia utotoni kuichezea klabu ya Real Madrid.

Hazard aliondoka Chelsea kwa kuwaachia zawadi ya magoli 21 kwa michuano yote ya msimu uliopita. Jitihada zake ziliwasaidia Cheslsea kujikongoja kumaliza nafasi ya tatu kwenye EPL na kushinda taji la Ligi ya Europa.

Kusepa kwa staa huyu mwenye umri wa miaka 29 sasa kuliwapa wakati mgumu zaidi kwa klabu ya Chelsea ambao walikumbwa na zuio la usajili kwa madirisha mawili kwa wakati huo kutokana na kukiuka taratibu za usajili. Meneja Maurizio Sarri pia alitimkia Serie A na wapo chini ya Frank Lampard sasa.

Katika kuamini kuwa Chelsea hawatapata mbadala wa Hazard kwa sasa, Didier Drogba alisisitiza kuwa klabu ya Cheslea walifaa kutafuta namna nyingine ya kusonga mblele bila Hazard ambaye aliingia Chelsea toka mwaka 2012.

Kwa Drogba, Chelsaea hawataweza kupata mtu wa kufanya maajabu kama Hazard, na kama ikitokea atakuwa aina ya mchezaji mwingine lakini siyo mbadala wa jumla wa Hazrd, japokuwa ukweli mchungu ni walilazimika kusonga mbele na wakasonga mbele.

“Hakuna wakuchukua nafasi ya Hazard. Yeye ni Spesho. Lakini mtu mwingine tu atakuja na kujitokeza. Hazard ni shujaa wa Chelsea. Haya ndiyo maisha, ndiyo soka” –Drogba

 Frank Lampard anatarajia kufanya mambo mengi makubwa katika kuboresha kikosi chake, anaamini amefanikiwa kuziba baadhi ya mapengo, lakini kazi bado inahitajika, sana.

7 Komentara

    Kiukwel tokea aondoke harzard Chelsea hakuna kitu

    Jibu

    maskin Chelsea

    Jibu

    Majanga

    Jibu

    Harzard fundii chelsea lazima wayumbe..

    Jibu

    Kwel kabisa hasaivi hamna kabisa yan mbovu sio Chelsea ya zamani sasa imekuwa hovyo

    Jibu

    Mbadala wa hazard hakuna kweli

    Jibu

    Club kubwa kuliko mchezaj

    Jibu

Acha ujumbe