Pep Abwaga Manyanga Usaili wa Mshambuliaji

Ndio kusema Pep Guardiola amekata tamaa au City wameondolewa kwenye ramani ya kumpata mrithi wa Aguero msimu huu? Hakuna usajili wa mshambuliaji, 2021/22.

Man City walikuwa sokoni kutafuta mrithi wa Sergio Aguero baada ya mchezaji huyo kuondoka City. Miongoni mwa wengi, Harry Kane na Erling Haaland ni wachezaji wawili waliohusishwa na City.

Kwa Kane, City waliripotiwa kutoa £100M ili kuipata saini ya nyota huyu wa Spurs. Pamoja na dau hilo, Spurs waliwatolea nje City wakisisitiza thamani yake ni £150M lakini pia hawana mpango wa kumuuza Kane.

Kutokana na hali ya kiuchumi iliyopo kwa sasa, Man City wamejiondoa kwenye kinyang’anyiro hiko na Pep amethibitisha kuwa haoni wakisajili mshambuliaji kwa msimu ujao.

“Kwa gharama tulizopewa, hatutonunua mshambuliaji, hatuwezi kumudu. Kila timu inataabika kiuchumi, hata sisi ni hivyo. Tuna Gabriel Jesus na Ferran Torres, walifanya vizuri kwenye nafasi hii.

“Tunawachezaji wengi kwenye akademi na mara nyingi tumecheza bila namba 9. Kuna nafasi kubwa hatutanunua mshambuliaji kwa msimu ujao.” 


KUSANYA PESA HAPA!

IcyGems kupitia Kasino ya Mtandaoni ya Meridianbet. Ndio, ukiwa kwenye nyumba ya mabingwa, ndipo utakapoufurahia ubora wa Kasino ya Mtandaoni sambamba na kushinda kwa ushindi mkubwa! Ishi na hii, IcyGems!Meridianbet

INGIA MCHEZONI

Acha ujumbe