Kocha wa Manchester City Pep Guardiola anaelewa hisia za Mauricio Pochettino baada ya kocha mkuu wa Chelsea kuingia uwanjani badala ya kupeana mikono na Mhispania huyo baada ya mechi yao.
Cole Palmer aliokoa pointi kwa wenyeji dakika za jioni akipiga mkwaju wa penalti baada ya Ruben Dias kumchezea rafu Armando Broja.
Aviator, poker, Roullette, Wild Icy Fruits, Piggy Party na mingine kibao upige pesa na Meridianbet. Ingia www. meridianbet.co.tz.
Na Guardiola amesisitiza kuwa hana hisia kali dhidi ya Pochettino ambaye alikabiliana na mwamuzi huku The Blues wakitaka kusawazisha kabla ya kipyenga cha mwamuzi huyo.
Alisema: “Sio tatizo. Ni sawa. Hisia hunitokea wakati mwingine. Sawa kabisa. Tangazo zuri kwa Ligi Kuu. Tulikuwa na wakati, walikuwa na wakati. Ubora walio nao, wanakupeleka kwenye ngazi nyingine kufanya maamuzi, sasa hivi nadhani ni matokeo ya haki.”
Pep aliendelea kusema kuwa kama unatarajia wanakuja pale na kushinda 7-0 basi wamekosea. Siku zote anatoa sifa kwa wapinzani na kila mtu anataka kuwashinda.
Beti na Meridianbet kwa odds kubwa na machaguo kibao, pia unaweza kubashiri mubashara.
Sura yao ni nzuri sana. Inatokea, unatoa sifa kwa timu zote mbili na Pochhettino atatoa uchambuzi kuhusu timu yake. Ilikuwa ngumu na matokeo ya haki.
“Hakuna cha kupoteza kwao. Chelsea ikishindwa na Man City watu wanasema ni kawaida, hakuna cha kupoteza lakini kwanini usiwape sifa Chelsea, wamefanya nini sokoni na watakuwepo na misimu ijayo atakuwepo.”
Ulikuwa mchuano mkali huko Stamford Bridge na kocha mkuu wa zamani wa Barcelona aliendelea kusifu ubora wa Chelsea walio nao ndani ya kikosi chao.
Aliongeza: “Unadhibiti eneo la kati, kwa hivyo unadhibiti mchezo. Lakini wana hawa watu Conor Gallagher, Moises Caicedo, Enzo Fernandez, Cole, na Raheem Sterling waliingia tena. Ni timu nzuri sana kwa hivyo hakuna shaka. Liverpool hawakuweza kushinda.”
Chelsea walikuwa bora zaidi kuliko Arsenal na mwisho, Arsenal walitoka sare. Kwa hivyo unajua, ni Chelsea, hawataondoka.