Pep Amjibu Klopp Juu ya Kauli Yake.

Kocha wa Manchester City Pep Guardiola amemjibu kocha mwenzake wa Liverpool juu ya kauli yake ya ukosoaji ya kuwa City wanatumia pesa nyingi kwenye kufanya usajili wa wachezaji.

 

Pep Amjibu Klopp Juu ya Kauli Yake.

Klopp siku si nyingi kabla ya kuvaana na timu hiyo ya Etihad alisema kuwa kwasasa hakuna timu ambayo inaweza kujilinganisha na City pamoja na Newcastle kwani wao wana pesa nyingi na kwa upande wa timu ya Guardiola wao wana wachezaji wenye ubora zaidi.

Klopp alitolea mpaka mfano wa wachezaji huku akimzungumzia Erling Haaland ambaye sasa ndio kinawa wa mabao katika ligi kuu ya Uingereza Kevin De Bruyne na wengine wengi.

Kutokana na kauli hiyo Pep aliibuka na kusema kuwa sio jambo la kushangaza kwasababu sio mara ya kwanza kwa kocha huyo kusema hivyo, amewahi kuzungumza mara nyingi juu ya matumizi ya pesa kwa Manchester City.

Pep Amjibu Klopp Juu ya Kauli Yake.

Guardiola baada ya kupoteza mchezo uliopita dhidi ya Liverpool kwa bao 1-0, ameendelea kusalia kwenye nafasi ya pili ya msimamo akiwa na pointi 23 nyuma ya pointi 4 dhidi ya vinara Arsenal.

Wakati Majogoo wa Anfield wao baada ya ushindi uliopita wamefikisha pointi 17, wakiwa nyuma ya pointi 10 kwa The Gunners ambao wapo kileleni huku nafasi yao ya kutetea taji hilo la ligi kuu Uingereza kuwa finyu.

Pep Amjibu Klopp Juu ya Kauli Yake.

 

Acha ujumbe