Pep Ampigia Saluti Bernado Silva Baada ya Kiwango Kizuri Kwenye Derby Jana

Pep Guardiola amemtaja Bernardo Silva kama mchezaji bora na pengo lake halitazibika baada ya kuonyesha kiwango kizuri wakati Manchester City ikishinda 3-0 kwenye mchezo wa derby dhidi ya Manchester United.

 

Pep Ampigia Saluti Bernado Silva Baada ya Kiwango Kizuri Kwenye Derby Jana
 

Kiungo huyo wa kati wa Ureno alikuwa katika hali ya kuvutia Old Trafford, akiunganisha krosi ya kupendeza kwa Erling Haaland bao la pili katika mechi hiyo jana.

Silva alihusishwa sana na kuondoka Etihad msimu uliopita wa joto kabla ya mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 29 kutia saini mkataba mpya wa miaka mitatu kusalia na vijana hao wa Guardiola.

Kuhusu kiungo wake nyota, Guardiola aliiambia Sky Sports: “Ninaweza kukaa hapa na kuzungumza kwa dakika 10 kuhusu Bernardo Silva anamaanisha nini kwangu na kwa timu yetu. Yeye ni mchezaji ambaye ni zaidi ya ubora katika idara zote mshikamano, akili, anaelewa kila kitu.”

Pep Ampigia Saluti Bernado Silva Baada ya Kiwango Kizuri Kwenye Derby Jana

Pep aliongeza kuwa, wanampenda sana, tatizo hana magari makubwa, anavaa labda si kwa staili ya juu. Yeye ni mnyenyekevu na kila mtu anampenda kwenye chumba cha kubadilishia nguo. Walikuwa na bahati ya kutompoteza hawezi kuondoka

Silva alifurahishwa na ushindi huo wa derby baada ya City kupata ushindi wao wa pili mfululizo kufuatia kushindwa na Arsenal na Wolves mapema mwezi huu.

Alisema: “Ulikuwa mchezo mzuri kwetu. Mbali na mipira michache tuliyopoteza, hatukuweza kuwapa nafasi kubwa ya kukabiliana nayo. Dakika 30 za kwanza za kipindi cha pili, tulikuwa wazuri sana. Jinsi tulivyokandamiza, tulichokosa dhidi ya Arsenal, tulikuwa wa ajabu.”

Pep Ampigia Saluti Bernado Silva Baada ya Kiwango Kizuri Kwenye Derby Jana

Hakika ni moja ya ushindi bora zaidi. Kushinda 3-0 ugenini, pamoja na umati huu, nadhani ni moja ya uchezaji bora. Alisema mchezaji huyo.

Acha ujumbe