Pep: Foden is the Greatest Talent

Mbele ya waandishi wa habari na kingereza chake cha kuokota Pep Guardiola akasema, “Phil Foden is the greatest talent I have ever managed”. Hakuna aliyemuelewa Pep Guardiola, hata mimi sikumuelewa.

Subiri kwanza, huyu ndiyo mtu aliyempandisha Messi kutoka La Masia pale Barcelona, huyu mtu amemfundisha Andres Iniesta, huyu mtu anafanya kazi na David Silva na Kelvin De Bruyne. Anamaanisha kweli kuhusu Foden??

Messi na Pep

Labda kingereza kinampiga chenga, labda lugha ya malkia inamkataa, labda alitaka kuzungumza vingine lakini tulimuelewa tofauti kwasababu hii si lugha yake ya kwanza.

Lakini hapana Pep Guardiola hakuwa na masihara, alikuwa anamaanisha. Siku David Silva anatangaza kuondoka Pep Alirejea tena kusema, msiniulize namsajili nani kuziba nafasi ya Silva, pengo la Silva tumeshaliziba, yupo Phil Foden, ana kipaji kuliko David Silva.

Hakuna aliyemuelewa tena, tulijua tu ni Pep na zile stori zake za kumkataa Toni Kroos kwasababu anapenda sana kufunga kutokea mbali badala ya kupiga pasi za mwisho kwa washambuliaji. Hakuna aliyewahi kumuelewa Pep.

Pep na Toni Kroos

Siku zinaenda na muda haugandi, Foden kwenye kiungo cha Manchester City anasahaulisha kuwa David Silva ameondoka The Citizens na Kelvin de Bruyne yupo juu ya kitanda cha hospitali anapatiwa matibabu.

Phil Foden ana miaka 20, Pep alimzungumzia akiwa na miaka 17. Pep alitudanganya au kutuambia ukweli?? Tunaogopa kujibu kwasababu hakuna aliyewahi kumuelewa Pep.


TENGENEZA MKWANJA UKIWA NA MERIDIANBET 

Unaweza kuvuna mkwanja mrefu kadiri uwezavyo kupitia mchezo wa Gold n Rocks kwenye  kasino ya mtandaoni ya Meridianbet. Ni rahisi! Vigezo na masharti, kuzingatiwa.

SOMA ZAIDI

11 Komentara

    Pep yupo sahihi kabisa

    Jibu

    Vizuri

    Jibu

    Pep yupo sahihi kabisa

    Jibu

    Kijana yupo vizuri

    Jibu

    Yupo sahihi

    Jibu

    Foden anahitaji mentor kama Pep ili aendeleze kipaji chake. Vijana wengi hupoteza uwezo uwanjani kwa sababu ya mambo nje ya uwanja

    Jibu

    Yuko vzur sana

    Jibu

    Yuko poa sana

    Jibu

    Yuko sahihi

    Jibu

    Inapendeza

    Jibu

    Kasena hivi anamkubali sana foden

    Jibu

Acha ujumbe