Jack Grealish ni miongoni mwa wachezaji wanaokuja kwa kasi sana kwenye ulimwengu wa soka. Uwezo wake umekuwa ni gumzo kwa vilabu mbalimbali. Pep Guardiola anajambo lake.

Baada ya Grealish kuhusishwa zaidi na Manchester United kwenye dirisha la usajili lililopita, Aston Villa walishinda vita hiyo baada ya kufanikiwa kusalia kwenye EPL na wakamsainisha Grealish mkataba mpya wa miaka 5 kuendelea kubaki Villa Park mpaka 2025.

Thamani ya Grealish kwa wakati ule ilisemekana ni pauni milioni 85 lakini kwa mkataba mpya aliosaini, inasemekana dau lake limepanda na Villa hawatomuuza kwa dau la chini ya pauni milioni 100.

Kupitia gazeti la Independent, moja ya sababu iliyotajwa katika mchakato wa kumsainisha Pep Guardiola mkataba mpya – lilikuwa ni suala zima la usajili.

Inaaminika Pep Guardiola amekiri wazi kuwa City inahitaji kufanya mabadiliko makubwa kwenye kikosi chake na hivyo baadhi ya wachezaji wameekwa kwenye mpango wa Guardiola katika kutekeleza hilo ndani ya miaka 2 aliyoongeza mkataba.

Pep Guardiola, Pep Guardiola Anajambo Lake Kwa Grealish, Meridianbet
Harry Kane (kushoto) na Lionel Messi (kulia). (Photo Credit; Daily Express)

Jack Grealish, Harry Kane na Lionel Messi ni majina makubwa yanayopewa kipaumbele kwenye orodha ya wachezaji wanaohitajika na Guardiola katika kuunda kikosi kipya.

Imeripotiwa kuwa tayari Guardiola ameshawaelekeza viongozi wake wanaohusika na usajili kuhusu Grealish na anatazamia kuisaka saini ya muingereza huyo katika dirisha kubwa la usajili linalokuja baada ya msimu huu kumalizika.

Kevin De Bryune anatajwa kuwa miongoni mwa wachezaji waliopendekeza jina la Grealish na walifanya mazungumzo ya kina na Guardiola kabla ya kuufikia uongozi wa City na kuwaelekeza kufanya hivyo mapema iwezekanavyo.

Kwa upande wa Grealish, inaaminika watu waliopo karibu na mchezaji huyo wanaamini ni suala la muda tu tukizungumzia mchezaji huyo kujiunga na timu yeyote kubwa kwenye akitokea Aston Villa ambapo ndiyo timu aliyoanzia maisha yake ya soka na yupo hapo mpaka sasa.

Je, City watafanikiwa kuipata saini ya Grealish? 

Licha ya City kuhusishwa na Messi, Pep Guardiola alinukuliwa akimsihi mchezaji huyo kuendelea kubaki Barcelona na taarifa zilizopo ni kuwa timu hiyo imejiondoa katika mchakato wa kumsajili Messi kutokana na umri wake (33) na mshahara wake ni mkubwa (pauni milioni 100 kwa mwaka).


USICHELEWE KUKAMATA MKWANJA HUU!

Hadi 130,000,000 TSH Kutolewa kwa washiriki wa shindano la Playson Cashfall. Unaipata kwenye Kasino ya Mtandaoni ya Meridianbet Pekee. Jisajili sasa, kisha ingia mchezoni kabla ya Novemba 29.

Meridianbet Tanzania Casino

SOMA ZAIDI

20 MAONI

  1. Jack Grealish, jina kubwa linalopewa kipaumbele kwenye orodha ya wachezaji wanaohitajika na Guardiola katika kuunda kikosi kipya,Safi Sana grealish.

  2. jambo jema kubadilisha mazingira ingawa wakala wake au kikosi chake waangalie kwamba uchumi hasaivi hauko vizuri hivyo wasipandishe dau kubwa

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa