Kocha wa klabu ya Manchester City Pep Guardiola amegoma kumzungumzia mchezaji wa klabu Borussia Dortmund kuhusu taarifa za uhamisho ambazo zimekuwa zikizagaa kuwa klabu yake imeshafanya makubaliano na mchezaji huyo.

Kuna taarifa zimekuwa zikizagaa kuwa mchezaji huyo nyota wa kimataifa wa Norway, kuwa klabu ya Manchester City wamekubali kulipa kiasi cha £63million ili kuvunja mkataba wake, pia wamekubaliana na mchezaji kupitia wakala wake mshahara wa £500,000 kwa wiki.

Pep Guardiola
Pep Guardiola

Klabu ya manchester City wamekuwa wakihusishwa na nyota huyo kwa muda mrefu sasa, lakini kocha wa klabu hiyo Pep Guardiola hakutaka kuingizwa kwenye tetesi hizo.

Akiongea na waandishi wa habari, Pep Guardiola alipoulizwa kuhusu Haaland alisema, “sina jibu la swali lako.”

Akaongeze, “sina jibu kuhusu maswali hayo. Ninavitu vitu vingine vinavyonihusu na kazi kichwani mwangu kwa sasa, kuliko kufikilia nini kitatokea kwenye hii klabu kwa msimu ujao.”

Tokea aondoke mshambuliaji namba tisa Sergio Aguero kwenye klabu ya Manchester City, imekuwa ikutumia namba tisa kivuli kwa kuwachezesha baadhi wa viungo wake washambuliaji kama Phil Foden, Raheem na Jesus kama namba tisa.


VUNA MKWANJA NA AVIATOR

Maana halisi ya ushindi mkubwa unaipata katika kasino ya mtandaoni ya Aviator kutoka meridianbettz. Andaa kapu la ushindi wa mkwanja na beti kibao za BUREEE.

tetesi, Tetesi za Soka Barani Ulaya., Meridianbet

SOMA ZAIDI

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa