Baada ya kuongeza mkataba wa kuendelea kukinoa kikosi cha Manchester City. Kocha Pep Guardiola amesisitiza kuwa hakunamashaka yeyote kuhusu hatma ya Aguero.

Sergio Kun Aguero amekuwa muhimili mkubwa wa City tangu alipojiunga na timu hiyo akitokea Atletico Madrid nchini Hispania.

Mkataba wa Aguero unamalizika msimu huu na haijajulikana kama ataendelea kubakia kwenye kikosi cha miamba hiyo ya Etihad.

Pamoja na kuwa na msimu mgumu ulioambatana na majeruhi ya mara kwa mara, Pep Guardiola bado anaamini katika uwezo wa Aguero na anampatia heshima yake kama mchezaji aliyeleta mafanikio makubwa kwenye timu hiyo.

Pep Guardiola, Pep Guardiola “Hakunashaka na Hatma ya Aguero”, Meridianbet
Baadhi ya makombe aliyobeba Aguero akiwa na Manchester City.

Akizungumzia suala la uwepo wa Aguero kwenye timu hiyo, Pep Guardiola amesema ” [Aguero] atatupa uamuzi. Anastahili kufanya maongezi na klabu ili kufikia maamuzi ambayo ni sahihi zaidi kwake, kwa klabu na kwa kila mtu”.

Aguero anaendelea kushikilia usukani wa kuwa mchezaji anayeongoza kwa kuwa na magoli mengi kwenye klabu hiyo. Tayari wachezaji wenzake ambao walikuwa pamoja kwenye sehemu kubwa ya kuleta mafanikio kwenye timu hiyo, wameshaondoka.

Yaya Toure, Joe Hart, David Silva, Vicent Kompany, Micah Richards na Samir Nasri ni miongoni mwa wachezaji walioipa heshima Manchester City wakiwa sambamba na Sergio Kun Aguero.


USICHELEWE KUKAMATA MKWANJA HUU!

Hadi 130,000,000 TSH Kutolewa kwa washiriki wa shindano la Playson Cashfall. Unaipata kwenye Kasino ya Mtandaoni ya Meridianbet Pekee. Jisajili sasa, kisha ingia mchezoni kabla ya Novemba 29.

Meridianbet Tanzania Casino

SOMA ZAIDI

19 MAONI

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa