Licha ya kuuanza msimu kwa matokeo ya kusuasua, kocha wa Manchester City – Pep Guardiola amethibitisha kutosajili mchezaji yeyote mwezi Januari mwakani.

Unaweza ukamshangaa Pep Guardiola kwa kuliongelea hili ikiwa ni muda mfupi umebaki kabla ya dirisha dogo la usajili kufunguliwa mapema Januari 1, 2021. City bado wanahaha kwenye safu ya ushambuliaji kutokana na wachezaji wa nafasi hiyo kukumbwa na majeraha ya mara kwa mara.

City ya msimu huu, sio ile tuliyoizoea kwa misimu kadhaa iliyopita. Guardiola anakikosi ambacho hakina madhara kwa sasa. Japokuwa yeye mwenyewe anasema “tunakikosi kizuri kinachoweza kupambania makombe yote”

Baada ya kuulizwa kama watasajili mchezaji yeyote baada ya kumsihi Messi abaki Barcelona na yeye mwenyewe kusaini mkataba mpya wa miaka 2 kuendelea kukinoa kikosi cha Manchester City.

Pep Guardiola alijibu “Hapana, nina timu nzuri zaidi inayoweza kupambana kwenye kila mashindano”

Je, City hii itatoboa msimu huu ikiwa katika ubora tuliouzoea? Au Pep atafanya maajabu kwenye dirisha dogo la usajili na hii kauli ikatumika kama kuwaadaa wachezaji inaowataka?


USICHELEWE KUKAMATA MKWANJA HUU!

Hadi 130,000,000 TSH Kutolewa kwa washiriki wa shindano la Playson Cashfall. Unaipata kwenye Kasino ya Mtandaoni ya Meridianbet Pekee. Jisajili sasa, kisha ingia mchezoni kabla ya Novemba 29.

Meridianbet Tanzania Casino

SOMA ZAIDI

17 MAONI

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa