Meneja wa Manchester City Pep Guardiola ameita timu yake kama “malejendari” baada ya kutwaa taji la Ligi Kuu ya Uingereza kwa ushindi wa 3-2 nyumbani dhidi ya Aston Villa siku ya Jumapili.

City walikuwa nyuma kwa mabao 2-0 kuelekea robo ya mwisho pale Uwanja wa Etihad, lakini mabao mawili ya Ilkay Gundogan aliyetokea benchi, na upande wa Rodri ndani ya kipindi cha dakika tano yaliwasaidia kugeuza mchezo na kushinda. Hili ni taji lao la nne la Premier League ndani ya misimu mitano.

Akizungumza na mancity.com baada ya kutwaa taji la Ligi Kuu, Guardiola alisema:

“Sisi ni malejendi. Unaposhinda mara nne kati ya tano basi ni kwa sababu hawa ni watu wa kipekee sana. Tutakumbukwa.

“Niliwaambia ni jambo la kawaida, lakini unapaswa kulishughulikia. Oleksandr Zinchenko alitupa mengi katika kipindi cha pili. Tulifunga bao na kupata kasi na mashabiki wetu wakafanya mengine.”

Guadiola pia amepongeza juhudi za wapinzani wao Liverpool, akisema: “Sijawahi kuona timu kama Liverpool maishani mwangu. Najua ni ngumu, lakini walitusaidia kuwa timu bora msimu baada ya msimu.

“Tunataka kushinda. Nina hisia kwamba wapinzani ni wagumu na watakuwa wagumu zaidi msimu ujao. Leo sina nguvu ya kufikiria msimu ujao. Sisi ni mabingwa tena! Tutatetea taji letu tena na tena.”

City walimaliza msimu wa 2021-22 kileleni wakiwa na pointi 93, pointi moja pekee mbele ya Liverpool walio nafasi ya pili, ambao walishinda 3-1 wakiwa nyumbani dhidi ya Wolverhampton Wanderers Uwanja wa Anfield.


TENGENEZA FAIDA NA ZEUS ANCIENT FORTUNES

Una Kila sababu ya kufurahia wiki yako na kutengeneza mwaka huu uwe wa faida zaidi katika kasino zetu za mtandaoni za meridianbettz. Mchezo wa Zeus Ancient Fortunes unakuongoza kutekeleza hilo.

tetesi, Tetesi za Soka Barani Ulaya., Meridianbet

CHEZA HAPA

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa