Pep vs Tuchel, Part 1 Inaanza Wikiendi Hii.

Huu ni mwezi ambao tutashuhudia vita ya Pep Guardiola vs Thomas Tuchel mara mbili ndani ya mwezi mmoja. Kama ni sinema, hii ni sehemu ya kwanza (part 1).

Chelsea watawaalika Manchester City kunako dimba la Stamford Bridge jumamosi hii. Huu ni mchezo ambao Pep anahitaji ushindi ili atangaze ubingwa wa EPL wikiendi hii. Upande wa pili, Thomas Tuchel anahitaji ushindi ili kujihakikishia nafasi ya kumaliza kwenye nafasi ya 4 msimu huu.

Licha ya kuwa Chelsea wanamchezo wa fainali ya FA siku chache zijazo, bado anahitaji kujihakikishia nafasi ya kucheza Ligi ya Mabingwa msimu ujao kwani lolote linaweza kutokea kwenye mchezo wa soka.

Akizungumzia mchezo dhidi ya Chelsea, Pep Guardiola amesema “Kila mara nimekuwa nikisema, kombe la Premier League ni la muhimu zaidi. Tumebakiza michezo minne na ushindi mmoja, kesho tutajaribu kupata ushindi.

“Tutapofanikiwa kubeba ubingwa wa Premier League, tutaizingatia zaidi fainali ya Ligi ya Mabingwa.” 

Kwa upande wa Tuchel, anasema “Kama unacheza dhidi ya Pep, unakuwa unajua kabisa huo ni mchezo mgumu kwa sababu ni kocha wa timu kubwa za Ulaya. 

“Wapo mbali kwenye ligi, tofauti ya pointi ni kubwa lakini kama tulivyofanya kwenye nusu fainali ya FA, ni juu yetu kupunguza hiyo tofauti ndani ya dakika 90 kisha tutafanya vivyo hivyo kwenye fainali (Ligi ya Mabingwa vs Man City).”

City atatangaza ubingwa wikiendi hii mbele ya The Blues, au darajani patavunjika na City ataendelea kusubiri?


TENGENEZA FAIDA KUPITIA MCHEZO WA TITAN DICE UKIWA NA MERIDIANBET KASINO

Unapokuwa kwenye Kasino ya Mtandaoni ya Meridianbet, huna sababu ya kucheza kwa mashaka. Titan Dice, ni mchezo unaweza kukupatia mamilioni kwa mzunguko mmoja!

SOMA ZAIDI

10 Komentara

  Safi sana

  Jibu

  Sawa

  Jibu

  Nice

  Jibu

  Ngoja tuone Nani atakuwa mbabe kwa mwenzie

  Jibu

  Good

  Jibu

  Vizuri

  Jibu

  Sawa

  Jibu

  Kesho tunasubilia kumuona mbabe

  Jibu

  Mechi ya ligi itaonyesha taswira fainal ya uefa itavokua

  Jibu

  Nice

  Jibu

Acha ujumbe