Winga wa Arsenal, Nicolas Pepe ameomba msamaha kwenye mitandao ya kijamii baada ya kutolewa nje kwa kadi nyekundu katika pambano la Ligi Kuu la Arsenal dhidi ya Leeds United mwishoni mwa wiki.

Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 25 alipata kadi nyekundu mara moja baada ya kuchezea vibaya Ezgjan Alioski mapema katika kipindi cha pili na sasa atatumikia marufuku ya michezo mitatu katika Ligi Kuu ya Uingereza.

Pepe ameamua kuwasilisha msamaha wake kupitia ukurasa wake wa Instagram akijutia kwa matendo yake katika mkwamo wa bao.

“Nimeiangusha timu yangu katika wakati muhimu wa mchezo na hakuna visingizio kwa tabia yangu. Samahani sana na ningependa kuomba radhi kwa mashabiki, wenzangu, kocha wangu na kila mtu kwenye klabu.”

Pepe Aomba Msamaha kwa Kadi Nyekundu
Pepe aomba radhi kwa kadi hii.

Pepe anaendelea kugawanya maoni huko Arsenal na amekuwa na wakati mgumu kupata namba ya kuanza chini ya Mikel Arteta kwenye Ligi ya Premia, licha ya kuchaguliwa baada ya Reiss Nelson kwa mchezo wa Leeds.

Kwa sababu ya kuongezeka kwa shida ya majeruhi ya Arsenal, Pepe anaweza kupewa nafasi ya kujirekebisha Alhamisi wakati Gunners wakisafiri kwenda Norway kuvaana na Molde kwenye Ligi ya Uropa.


Usichelewe Kukamata Mkwanja Huu!

Hadi 130,000,000 TSH Kutolewa kwa washiriki wa shindano la Playson Cashfall. Unaipata kwenye Kasino ya Mtandaoni ya Meridianbet Pekee. Jisajili sasa, kisha ingia mchezoni kabla ya Novemba 29.

Meridianbet Tanzania Casino

SOMA ZAIDI

21 MAONI

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa