Peter Kenyon katika Safari ya Senzo Mbatha

2004 Old Trafford Kaskazini Mashariki mwa England, haukuwa usiku mzuri sana kwa Peter Kenyon, kwenye mtanange wa Manchester United na Chelsea, Mashabiki wa timu zote mbili walikuwa wanamzomea Peter Kenyon

Ni nani huyu Kenyon? Huyu alikuwa Mtendaji Mkuu wa United kabla hajaondoka na kutua Chelsea, inasemekana aliondoka na faili muhimu la sajili za United, akaenda kulitumia Chelsea ikiwemo saini ya Jose Bosingwa, ilikuwa ni mpango wa United

United walimzomea kwasababu waliamini kawazunguka sana, ikiwemo mipango muhimu ya usajili yote akaenda kuifanya akiwa na Chelsea, wakati Mashabiki wa Chelsea wanamzomea Kenyon ni kutokana na kumtimua Claudio Ranieri pale Darajani, wakasema wazi “Peter you are public enemy”

Mashabiki wa Arsenal pia walimchukia, mwisho Taifa zima lilimchukia, inasemekana kwenye saini ya Ashley Cole kutoka Arsenal kwenda Chelsea, Cole alikuwa na wakala wake Pini Zahavi mgahawani, Kenyon na Mourinho walifika pale baada ya mazungumzo machache dili likaisha

Hii inanikumbusha nchini Tanzania, namkumbuka CEO wa Simba Senzo Mbatha, anaweza kua anapitia script moja kama ya Kenyon, aliondoka Simba bila watu kutarajia akavuka upande wa pili bila watu kutarajia na kusaini zinafanyika ambazo hazikutarajiwa

Unaweza kumpa jina Senzo kama Transfer Guru, moja kati ya watu wenye mikono ya dhahabu kwenye kunasa wachezaji, moja kati ya watu wenye mikono ya makombe, kule kwao wanamuita The Trophy Magnet, ni mtu mwenye damu na makombe

Bahati mbaya sana watu hawajui kuwa mpango wa klabu kwa msimu mpya hufanywa na watu muhimu sana klabuni kama Senzo, kama Kenyon pia alivyopewa nafasi pale United, wote walijua timu zao zinataka kufanya nini, zina nguvu gani na udhaifu gani

Tofauti tu ni kuwa Senzo hatozomewa na Yanga huku Tanzania, utamzomea vipi kama amekupa ramani ya kwenda Congo, amekupa ramani ya Afrika Magharibi, amekupa ramani ya yule Mrundi, mwisho wa siku atazichanga vyema karata kuhakikisha wanabeba ubingwa wao

Tunaweza kuwaita Maadui, ila tuwaheshimu tu kwakuwa waliupenda Mpira, mpira ukawapenda, wakaenda darasani kuusoma mpira, AN ENEMY YET A FRIEND


VUNA SHEA YAKO YA 230,000,000TSH NA UFURAHIE MSIMU HUU WA SIKUKUU!!!

Kupitia Kasino ya Mtandaoni ya Meridianbet, jiwekee nafasi ya kupata shea yako ya 230,000,000Tsh kupitia mchezo wa Secret Santa. Hakika hutojutia kufurahia msimu huu wa sikukuu ukiwa katika nyumba ya mabingwa ya Meridiabet. Unasubiri nini???

SOMA ZAIDI

10 Komentara

    Tunaishi nao tu hawa wanafik

    Jibu

    Kenyon hakufanya vizuri hilo ni funzo la kuishi na watu kwa umakini mkubwa

    Jibu

    Ni ni aibu kubwa kwa kenyon

    Jibu

    Kenyon hatari

    Jibu

    Duuuh noma sana hii

    Jibu

    Kenyon ni noma

    Jibu

    Kenyon ni balaa

    Jibu

    Kenyon atari

    Jibu

    Kenyon nomaa

    Jibu

    Sijawahi ona mtu mnafiki kama senzo

    Jibu

Acha ujumbe