Mkurugenzi wa masuala ya ufundi, na mshauri wa klabu ya Chelsea, Petr Cech ametangaza kuondoka baada ya kuitumikia nafasi hiyo tangu 2019, alipotokea Arsenal kama mchezaji.

Kipa huyo wa zamani wa Chelsea anaungana na Marina Granovskaia, pamoja na aliyekuwa Mwenyekiti wa klabu hiyo Bruce Buck waliotangulia kutangaza kuondoka.

Mabadiliko ya uongozi Chelsea yameanza tangu ujio wa bilionea mpya Todd Boehly, aliyenunua klabu hiyo baaada ya kuuzwa na Roman Abramovich.

Akizungumza baada ya kuthibitisha kuachana na Chelsea, Cech amesema anajivunia kufanya kazi kama mshauri na mkurugenzi wa mambo ya kiufundi wa klabu hiyo, aliyodumu kwa muda wa miaka mitatu.

 

petr cech, Petr Cech Atangaza Kuondoka Chelsea., Meridianbet

“Limekuwa jambo la kujivunia sana kutumika kwenye nafasi hii ndani ya Chelsea. Kutokana na klabu kuwa chini ya umiliki mpya lakini nafikiri kwangu ni muda sahihi kuondoka.”

“Ninafuraha kwamba kwasasa klabu ipo kwenye hali nzuri ikiwa na wamiliki wapya na nina amini itakuwa na mafanikio makubwa ndani na nje ya uwanja.”

Mmiliki wa Chelsea, Todd Boehly amezungumzia kuhusu kuondoka kwa Petr Cech akisema ni mtu muhimu ndani ya klabu hiyo.

“Petr ni mtu muhimu ndani ya familia ya Chelsea.”

“Tunaelewa uamuzi wake wa kuamua kuondoka na tunamshukuru kwa ushirikiano wake na majukumu yake aliyoyatimiza kama mshauri na uwepo wake. Tunamshukuru sana.” alisema Boehly.

Kwa mujibu wa taarifa, Todd Boehly alitaka Petr Cech asalie klabuni hapo kutokana na uzoefu wake lakini Cech mwenyewe ndiye aliyefanya maamuzi ya kuondoka.


ALIYA’S WISHES

Bila shaka unatamani ushindi mkubwa, vipi kuhusu kujaribu Sloti hii ya Aliya’s Wishes? jaribu ushinde sasa.Kasino ya Mtandaoni

CHEZA SASA

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa